Serikali imeombwa kuingilia kati na kutatua umiliki wa makao ya watoto ya Good hope Mtito Andei
26, Jan 2021
Serikali imeombwa kuingilia kati ili kutatua mzozo unaoukumba umiliki wa makao ya watoto ya Good Hope yaliyopo eneo la Mtito Andei. Kulingana na usimamizi uliopo, inadaiwa ya kwamba makao hayo yaliyojengwa na mfadhili kutoka ujerumani na yalikuwa yawasaidie watoto kutoka familia zisizojimudu na wale wa kurandaranda mitaani lakini sasa kwa sababu ya mvutano idadi kubwa ya watoto hao wanataabika na hata kukosa elimu.