×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

IEBC yasisitiza kwamba haitabadili orodha ya viongozi walioteuliwa

News

Tume ya Uchaguzi nchini IEBC imesisitiza kwamba haiwezi kubadili orodha ya watu walioteuliwa na vyama mbalimbali kujaza nafasi za wawakilishi wadi na wabunge maalum katika Bunge la Kitaifa na Seneti.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati uteuzi huo uliofanywa kwa mujibu wa sheria ambapo vyama vyote viliwasilisha majina kwa IEBC kabla ya uchaguzi.

Kadhalika amefafanua kwamba idadi kamili ya walioteuliwa kupitia vyama mbalimbali ilibainika baada ya uchaguzi kwa kutumia mfumo wa wazi kutegemea na idadi ya watu waliochaguliwa kupitia vyama hivyo.

Kwa mujibu wa mchakato huo, IEBC imesisitiza kwamba njia ya pekee ya kubadili jina ni kupitia kuwasilishwa kwa kesi mahakamani.

Ikumbukwe, kumekuwa na malalamishi kutoka kwa wanachama wa vyama mbalimbali kuhusu watu waliochaguliwa, wengi wakilalamikia kuachwa nje ya orodha ya mwisho iliyochapishwa katika gazeti rasmi la serikali.

Haya yanajiri huku watu wenye ulemavu katika Kaunti ya Trans Nzoia wakipiga kambi nje ya ofisi ya Tume ya Uchaguzi IEBC kwa takribani saa moja kulalamikia kuwachwa nje kwenye orodha ya wakilishi wadi walioteuliwa na vyama mbalimbali.Mwenyekiti wa kundi lao, Odhiambo Opis na mshirikishi, Tom Juma kwa pamoja wametishia kuwasilisha kesi mahakamani kuwazuia wakilishi wadi wa kaunti hiyo kuapishwa siku ya Jumatano juma lijalo.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week