×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

William Kipchirchir Samoei Ruto ndiye Rais watano wa Kenya!

News

William Kipchirchir Samoei Ruto ndiye Rais Mteule wa tano wa Kenya. Ruto ameibuka mshindi baada ya kupata kura milioni saba, elfu mia moja sabini na sita mia moja arobaini na moja. Ushindi huo ni wa asilimia 50.49.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, IEBC Wafula Chebukati amemtangaza Ruto mshindi huku Raila Odinga wa Azimio akiibuka wa pili kwa kura milioni sita, elfu mia tisa arobaini na mbili, mia tisa thelathini ambayo ni asilimia 48.85. George Wajakoya wa Chama cha Roots ameibuka watatu kwa kura elfu sitini na moja, mia tisa sitini na tisa huku Waihiga Mwaure wa Chama cha Agano akiibuka wanne kwa kura elfu thelathini na moja, mia tisa themanini na saba.

Kulingana na matokeo hayo ina maana kwamba hakutakuwa na duru ya pili ya urais kwani mshindi amepata asilimia zaidi ya hamsini na kura moja imeafikiwa..

Akitoa tangazo hilo, Chebukati amesema kwamba licha ya vitisho na hata kujeruhiwa kwa makamishna wawili wa tume hiyo na wengine kutoweka katika hali za kutatanisha, ametekeleza jukumu lake la kikatiba la kutangaza matokeo ambayo ni ya mwisho kwake yeye kutangaza kabla ya hatamu yake ya uongozi kukamilika.

Akizungumza baada ya kutangaza mshindi, Rais Mteule, William Ruto ameipongeza IEBC kuhusu namna ilivyoendesha uchaguzi akisema shughuli hiyo ilifanyika kwa uwazi, kwani matokeo yaliwekwa katika wavuti wa IEBC ili kutoa nafasi kwa umma kuyadurusu.

Ruto aidha amesema kwamba licha ya mahangaiko na msukosuko wa kisiasa aliyopitia, wapiga-kura walifanya uamuzi na kumpa ushindi huku akiahidi kuwa Rais wa wote hata waliokuwa mahasidi wake wa kisiasa.

Pia amempongeza Rais Uhuru Kenyatta anayeondoka madarakani kwa kipindi ambacho wamekuwa naibu wake na kuahidi kutimiza maono waliokuwa nayo walipobuni serikali mwaka 2013.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week