×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Alfred Mutua Atangaza kumuunga mkono Wavinya Ndeti

News

Gavana wa Machakos Alfred Mutua ambaye pia ni mmoja wa vigogo wa muungano wa Kenya Kwanza, ametangaza kumuunga mkono Wavinya Ndeti wa WIPER katika kinyang'anyiro cha ugavana katika kaunti hiyo, siku chache tu baada ya Naibu wake kujiondoa katika kinyang'anyiro hicho na kutangaza kumuunga mkono Wavinya Ndeti.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa UDA huko mjini Machakos, Mutua ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Maendeleo Chap Chap, amesema ana Imani na uongozi wa Ndeti.

Tangazo la Gavana Mutua kumuunga mkono Ndeti wa WIPER, limeibua mjadala kuhusu utata wa umoja wa viongozi wa Ukambani, hasa ikizingatiwa kwamba Mutua amemuunga Ndeti ambaye ni wa mrengo tofauti badala ya kumuunga Jonshon Muthama wa UDA ambaye pia alihudhuria mkutano huo.

Wakati uo huo, Mutua amewahimiza wakazi wa eneo la Ukambani kumchagua William Ruto kuwa Rais, akisema ana matumaini kwamba Naibu wa Rais atalinda maslahi ya Jamii ya Akamba iwapo atashinda urais.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week