×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Amin Mohamed Ibrahim ndiye Mkurugenzi mpya wa DCI

News
Amin Mohamed Ibrahim ndiye Mkurugenzi mpya wa Idara ya Upelelezi, DCI baada ya kuteuliwa rasmi na Rais William Ruto. Uteuzi wa Amin umechapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali. Kabla ya uteuzi wake,  Amin alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa masuala ya Ndani katika Idara ya Polisi internal Affairs Unit IAU.

Kabla ya hapo alikuwa msimamizi wa kitengo cha uchunguzi katika makao makuu ya DCI. Amewahi kuhudumu katika vitengo vingine mbalimbali kama kile cha upelelezi wa uhalifu wa kifedha .

Alipandishwa cheo na kuwa Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi Mwezi Machi mwaka jana. Uteuzi wa Amin umefanyika baada ya jumla ya watu kumi waliorodheshwa kwa mchujo kuhojiwa wiki iliyopita. Waliohojiwa ni Bernard Barasa Walumoli, Eliud Kipkoech Lagat, Gideon Nyale Munga, Esther Chepkosgei Seroney na David Kipkosgey Birech. Wengine ni Jonyo Michael Wiso, Nicholas Ireri Kamwende, Paul Jimmie Ndambuki na Simon Mwangi Wanderi.

Amin anachukua nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa DCI, George Kinoti. Kujiuzulu kwake kulitangazwa na Rais William Ruto huku Hamisi Massa akiteuliwa kuhudumu katika wadhifa huo kikaimu kabla ya kutangazwa kwa Mkrugenzi  mpya. 

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week