Wiki moja tangu shughuli ya kubaini uwezo wa chanjo dhidi ya virusi vya HIV HVTN 702 kusitishwa na kuwavunja moyo wengi waliodhania hatimaye mbinu mwafaka ya kuzuia maambukizi imebuniwa, wanasayansi na watafiti wa chanjo hiyo wamehakikisha kuwa bado kunamatumaini ya kubuni chanjo nyingine itakayosaidia pakubwa katika kuzuia maambukizi.
Chanjo hiyo ilisitishwa kwa misingi kuwa haijafikia viwango vya kuzuia maambukizi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kitaifa ya Chanjo dhidi ya Virusi vya HIV, Daktari Kundai Chenyenze, matumaini yapo kwani majaribio bado yanaendelea katika mataifa mbali mbali.
"Hatujafa moyo, kama watafiti tunaendelea na mikakati ya kuhakikisha chanjo dhabiti inapatikana, tumejifunza mengi kutokana na utafiti huo na tutahakikisha tunabuni chanjo kamili na ya bei nafuu itakayopunguza maambukizi ya HIV."
Kauli sawa na hiyo ilitolewa na mmoja wa watafiti wakuu katika taasisi ya IAVI Profesa Omu Anzala, amabaye amesisitizia umuhimu wa kupimwa na matumizi ya dawa ya PEP zinazozuia maambukizi.
Mjaribio ya chanjo hiyo ya HVTN 702 maarufu Uhambo trial yalifanyika katika taifa la Afrika Kusini kunzia mwaka 2016 ambapo watu 5,407 walijitokeza kufanyiwa majaribio.
Watu hao waliochaguliwa walikuwa wakiume na wakike walio kati ya miaka 18 na 35, vilevile wanoshiriki ngono.
Daktari Chenyenze anaeleza kuwa baadhi ya waliofanyiwa majaribio waliambikizwa virusi hivyo sababu kuu iliyosababisha chanjo hiyo kusitishwa.
- Man receives first eye transplant in step toward one day restoring sight
- A journey of empowerment: Nurturing youth via age-appropriate human sexuality education
- Food security: Kenya's long debate on GMOs far from over
- Tuberculosis remains one of world's deadliest diseases, but hope for vaccine rises