Kenya sasa tunajivunia na kusherehekea ushindi wa mwanadada aliyetwaa ubingwa wa Miss Intercontinental Kenya mwaka huu 2017.

Ni baada ya zoezi nzima na shughuli pevu ya kuwania nafasi hio ambapo mwanadada huyo kwa jina Sheila Rono amelitwaa taji maarufu duniani.

Tamasha hilo lilofanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 28, July 2017 ndani ya ukumbi wa Radisson Blu Hotel, Upperhill Nairobi, lilifana kwani watu mashuhuri walihudhuria kumpa hongera lakini pia kumtawaza mshindi wa taji hilo.

Aliyekuwa Miss Intercontinental Kenya, Brenda Chebet Juma, na anayeishi Ujerumani kwenye shughuli zake za kimaisha na masomo, ndiye aliyekuja kumvisha taji hilo Jumamosi.

Sheilah, atakuwa anawakilisha Kenya kwenye mashindano ya dunia nzima Mumbai India mwezi Novemba 2017.

-Na;MkazivaeUNIT

.

Keep Reading