×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Wasia- Ahmed Dharwesh's last poem

News

Huu ndo wangu wasia, naomba muutawili,

Imedhoofu afia, na kusawijika mwili,

Naona nakaribia, kukutana na jalali,

Wasia wangu ni huu, naomba zingatieni

 

Iwapo nitajifia, ruhu iitoke mwili,

Musije kunililia, kwa kufuata sabili,

Ni ada ya kidunia, mauti kuyakabili,

Wasia wangu ni huu, naomba zingatieni

 

Jambo nalotarajia, nifanzieni sahali,

Dhiki sitaki watia, wa kuukafini mwili,

Sanda ‘mejinunulia, hilo lisiwe muhali,

Wasia wangu ni huu, naomba ufuateni

Kama leo najifia, kwa yoyote ile hali,

Najua mutaumia, kunikosa ni thakili,

Ombeni sana jalia, anipe pema mahali,

Wasia wangu ni huu, naomba ufuateni

Mombasa kinifukia, nataraji wangu aali,

 

Pale nipokusudia, Kikowani musifeli,

Kwa nilowapa udhia,msamaha mukubali,

Wasia wangu ni huu, naomba uzingatieni

Ya kwamba sijatimia, kwenu nataradhalali,

Wanangu nawaachia, binti zangu wawili,

Muwe tanisaidia, masomoni wasifeli,

Elimu kiwapatia, nitapumzika kweli.

Rijali wangu kawadia, Ridhwan ndio lake jina,

Sito kuwa nawe sikia, mlezi wako mama,

Mke wangu maridhia, Bihawa lake jina,

Mola takujalia, Subira ilo jamila.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week

.

Similar Articles

.

Recommended Article