BBI: Ni msitu mpya, nyani ni wale wale

Ni ripoti iliyongojewa kwa hamu kubwa na wananchi huku viongozi wanaoipinga na wale wanaounga mkono wakianza kulumbana kuhusu hatima yake hata kabla ya kujadiliwa rasmi kwa umma.

Wakenya nao wamejiunga na viongozi wao kwenye mjadala huu katika mitandao ya kijamii.

Na kama viongozi walivyogawanyika makundi matatu, moja likipinga kubwagiwa umma kwa kura za maoni, la pili likiuunga mkono ijadiliwe bungeni, nalo kundi la tatu likitaka kwanza lisome ripoti kamili kabla kutoa maamuzi ya aidha kukabiliwa wataalam wa kikatiba kuikarabati kuwa mswada wa kuazimia kura ya maoni.

Ripoti ya BBI imezua mjadala mkubwa huku, malumbano yakizuka mabarazani na katika mitandao ya kijamii na hata kuwalazimu wasimamizi wa mitandao kutandaza mabango yenye misemo kama vile ‘Form ni BBI’, ‘Say No to BBI’ ama kataa BBI, kama njia ya kuwavutia wakenya kupinga ama kukataaa ripoti hiyo.

Ripoti ya BBI imetolewa wakati ambapo miaka miwili tu imesalia Kenya kuandaa uchaguzi mkuu wa tatu chini ya katiba ya mwaka 2010.

Kwa vingozi wakuu wa kisiasa, kinyanganyiro cha kufanikisha mageuzi kwenye mapendekezo ya ripoti ya BBI au kuiangusha kunabeba uzito mkubwa katika hatima yao ya kisiasa.

Kwake Rais Kenyatta anayeipigania ili aweza kuacha kumbukumbu njema kwa taifa la Kenya, anaonekana kujitolea kuwashawishi Wakenya kumuunga mkono ili kufanikisha utekelezwaji wa mageuzi ya kikatiba yatakayohakikisha kwamba machafuko ya kisiasa kila baada ya uchaguzi mkuu hayatokei tena siku za usoni.

Hata ingawa Rais anaonekana kupigana na shinikizo kutoka kwa wandani wake kutoka eneo la kati kwamba ana nafasi nyingine ya kusalia uongozini baada ya muhula wake wa pili kukamilika miaka miwili ijayo, anaonekana kupendelea wazo la kuendelea kuhudumu katika wadhifa wa Waziri Mkuu ambao umekosa makali kuambatana na ripoti hii ya BBI ijapo heuda kipengee hiki kikapigwa msasa wakati wa maamuzi mapya ya umma na kupitia kwa kura ya maoni inayopendekezwa na wengi.. Wapo viongozi kutoka eneo la kati hata hivyo wanaopendelea kuwepo kwa mageuzi kamili yatakayowaleta viongozi wapya serakalini.

 Kiongozi wa chama Cha Narc Kenya, Martha Karua amemuonya Rais dhidi ya kuwania tena uongozi wa nchi iwe kwenye mfumo wowote ule.

Muda wa kuhudumu uongozini umewekwa ili kuhakikisha kwamba yeyote yule anayehudumu katika wadhifa wa uongozi wa nchi hazidishi mda wa mihula miwili. 

“Ikiwa tutabadilisha katiba kubuni wadhifa wa waziri mkuu ambaye ni kiongozi wa serikali, mtu ambaye amehudumu kama rais basi, hawezi kuwa Waziri Mkuu, kwa hiyo namshauri kakangu Uhuru ambaye nimemuunga mkono na bado ninamuunga mkono amalize muhula wake, afahamu kwamba hayo mawazo aliyo nayo si sahihi kikatiba’’, amesema Karua. 

Katiba mpya ya mwaka 2010 inamlazimu kiongozi wa nchi kustaafu baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.

Kwa upande wake kiongozi wa upinzi Raila Odinga ambaye pia anapigania kuacha kumbukumbu atakapostaafu siasa ambazo amekuwa ndani kwa miongo minne kuanzia mwaka wa 1990 ameanza kuwatia hofu wafuasi wa Naibu wa Rais William Ruto wanaopinga kutekelezwa kwa ripoti ya BBI kwani wanaaamini kwamba itamfungia nje Ruto kwani tayari ipo picha inayoashiria kwamba ikiwa Uhuru atakuwa Waziri mkuu  wa  Urais na hivyo huku Ruto akikosa kutajwa popote na wandani wa Raila na Uhuru katika mfumo mpya baada ya mageuzi ya BBI.

Naibu wa Rais ameonekana kupaza sauti ya wanyonge kwa kutoa wito kupingwa kwa ripoti ya BBI kuregeshwa mashinani kwa maamuzi ya kura ya maoni akisema kwamba ni ishara ya kusumbika nafasi ya za uongozi kwa wachache ambao wamekosa kuwarai wapiga kura kuwapa nafasi ya kuwahudumia.

Kwenye mfumo wa uongozi wa chama cha ODM mwaka 2007 Raila alikuwa ametengewa nafasi ya Rais, Naibu wake akiwa ni Msalia Mdavadi huku William Ruto akitengewa nafasi ya Waziri Mkuu nafasi aliyopewa Raila baada ya mzozo wa matokeo ya uchaguzi mkuu huo uliosababisha umwagikaji mkubwa wa damu na uharibuifu wa mali.

Kumekuwa na ushindani usio na kifani baina ya Raila na Ruto na kila moja anonekana kukosa kumuamini mwenziwe katika mipango yoyote ya baadaye kuhusu uongozi wa nchi.

Wadadisi wa maswala ya kisiasa wana msemo kwamba Ruto pekee ana uwezo wa kumsimamisha Raila kutwaa uongozi wa nchi ambao amejibidisha sana kuu?kia bila mafanikio. 

Raila pia anao uwezo wa kumsimamisha Ruto kuwa rais mwaka 2022 kwani ruto alisababisha Raila kukosa ku? kia Ikulu mwaka 2013 na mwaka 2017 kwa kuchagua kujiunga na kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta. 

Uhasama huu kati ya Ruto na Raila umeonekana kukita mizizi baada ya uzinduzi wa ripoti ya BBI.

Ingawaje Ruto Na Raila wamekuwa wakiunga mkono mfumo wa bunge unaoongozwa na Waziri Mkuu.

Kwa muda wa hivi karibuni Naibu wa Rais ameonekana kubadilisha mtindo wa nyimbo zake za kisiasa na kupinga matamshi yote yanayonuia kuupigia debe mfumo wa Bunge.

Viongozi wengine wanaonuia kujijenga kwenye mjadala huu wa ropiti ya BBi na marekebisho ya kikatiba kwa kupinga au kuunga mkono ni pamoja na magavana Hassan Joho wa Mombasa, Wycliff  Ambetsa Oparanya wa Kkamega, Anne Waiguru wa Kirinyaga na Alfred Mutua wa Machakos miongoni mwa wale waliosimama kidete na Raila Odinga.  

Hao wameonekana kuchukua nafasi ya mbele kwenye mapambano haya ya kisiasa ya mageuzi na urithi wa Rais mwaka 2020.