× Business BUSINESS MOTORING SHIPPING & LOGISTICS DR PESA FINANCIAL STANDARD Digital News Videos Health & Science Lifestyle Opinion Education Columnists Moi Cabinets Arts & Culture Fact Check Podcasts E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wakurugenzi wa KPA waenda ugangani ili kukwepa pingu

COAST
By Ripota Wetu | Sep 25th 2019 | 4 min read
By Ripota Wetu | September 25th 2019
COAST

Imebainika wazi kuwa mkugugenzi wa upelelezi George Kinoti na mwenzake msimamizi mkuu wa mashitaka ya Serikali Noordin Haji watazidi kupiga guu na njia sana kuzuru bandari ya KPA na kurudi Nairobi labda kwa miezi mingi zaidi.

Washirikina ambao ni miongoni mwa wafanya kazi wa bandarini na wakaribu wa mameneja fulani wakuu, wanayo Imani kwamba waganga wao wameweza kuwakwepesha makubwa mbeleni hivyo suala la Kinoti na Haji kamwe halistahili waganga wa Sumbawanga ila hapa Pemba tu.

Wanasema afi si tatu za EACC, DPP na DCI zitasumbuka kwa muda hadi kesi hizo zinazowakabili mameneja wakuu wa KPA zitakapofi fi a kufuatia bumbuazi la uchawi ambao matapeli wanaotumika kuleta waganga na uganga wanaendelea kujigamba kwamba jua litatoka mawio hadi machweo bila ya mtu yeyote kukamatwa.

Yaaminika baadhi ya mameneja wenye wasi wasi na kimbuka cha madai ya ufi sadi hapo ndani, wameamua kuwatumia wafanya kazi wadogo walio wakaribu yao kuwatafutia waganga wa kuzima moto wa Kinoti na Haji.

Twaambiwa baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuwaambia mameneja wa KPA kwamba safari hii kila mtu ataubeba msalaba wake wa ufi sadi, kikao cha dharura kilifanyika na wahusika wakaamua kuchangia gari mfanya kazi mmoja ambaye alisaidiwa kama mkopo wa gari kulinunua ili kuweza kuwaleta na kuwasafi risha waganga kutuliza na kufyatua mori wa DCI, DPP na EACC.

Leo hii tunaarifi wa kuwa waganga kutoka kaunti kadha wa kadha wanaendelea kuvuna pato la dharura kutoka kwa mameneja waliojawa na wasi wasi mkubwa kwamba wakati wowote wanaweza kukamatwa kutokana na madai yanayozidi kuchipuka kila uchao.

Ushirikina katika bandari ya Mombasa umeanzia daraja la chini hadi ngazi za mameneja huku miaka ya nyuma kukiwa na matukio ya afisi kupatikana na zana za kiuganga ama tambiko zenye kuambatana na suala la urogi.

Fitina na usabasi imetajwa kuwa ni mazoea hapo na ripoti zaidi zasema huku wakijaribu mbinu hata za waganga, pesa pia zinatembea kila pembe katika jitihada zao za kung’oa vihunzi vya ufi sadi.

Wafanya kazi wa kitengo cha maakuli (Dock Workers Union) wanatajwa kuwa fungu la wale wengi wanaotumiwa baadhi yao kushirikishwa kwenye zoezi hili la ushirikina.

Paka chumbani

Uchunguzi wa kina unachomoza dalili za uwezekano wa ushirikina mwingi katika halmashauri ya bandari nchini kutokana na historia ya visa na visanga ambavyo vimewahi kushuhudiwa afi si nyingi humo pamoja na jinsi wakurugenzi wa awali kati ya miaka ya 1980s na 1990s walivyonaswa wakitumia ndumba kujiokoa.

Katika kisa kimoja cha miaka ya 1990s, mkurugenzi mmoja ama meneja mkuu wa halmashauri ya bandari nchini (KPA), aliponea chupu chupu kutoka kwa makucha yap aka mweupe ambaye alifungiwa chumbani na mganga wake na kumwamuru ahakikishe amemuua paka huyo ndio kesi inayomkabili pia ife fi i kama paka huyo.

“Mdosi alikuwa muoga kwa kuwa kung’ang’ana na paka chumbani siyo dhihaka. Mimi na mwenzangu tuliamua kumsaidia kukokota paka huyo tukiwa uchi wa mnyama hadi akafa,” asimulia mkaribu wake wa wakati huo ambaye kwa sasa uhusiano wao umegeuka wa paka na panya.

Kulingana na shahidi huyu (ambaye jina lake tumelibana), kweli walishirikisha zaidi ya waganga saba wa humu nchini nan chi jirani kuamini kwamba wangeweza kufi lisi kesi iliyokuwa inamwandama rafi ki yao na mdosi wao.

Wanasema kesi yake hatimaye iliyeyuka mfano wa barafu. Mtindo wa nguva Mbali na meneja huyo wa kisa cha paka, hatimaye kunaye mwingine wa KPA miaka ya 2000 ambaye alifaulu kukaa kwa vipindi fulani lakini kwa uaminifu wa juju na jujuvule.

Akisaidiana na meneja wake mdogo wa huduma za bandari wakati huo, yasemekana alikuwa na tabia ya kuwaleta waganga kutoka Pemba, Tanzania.

Siku moja, mdogo wake huyo alimleta mganga wa Pemba mapema sana lakini akakawia afi sini ama kumfi cha ofi sini mwake hadi machweo ya siku. Kufi kia mwendo wa saa tano usiku hivi, meneja huyo na mdogo wake mshiriki pamoja na mganga wao, walielekea kufanyia tambiko lao eneo la kiegezo cha Kipevu.

Wataalam wa masuala haya wanasema kwamba mshirikina anapomwamini mganga wake, huingia kimawazo mzima mzima kushinda vile Mkristu amheshimuvyo pasta wake ama mtume yeyote yule.

Hii ndio maana wengine wamepoteza maisha yao kwa kulishwa madawa yasiyo na utafi ti wowote ama kupotoshwa vilivyo na matapeli.

Nasema hivyo kwa sababu katika kisa cha mganga huyu, twaambiwa mteja wake aliamuriwa kuvua nguo zote pale Kipevu wakati huo na kuanza kuchanjwa mwili wote ilhali Mungu siyo Athumani, baadhi ya wafanya kazi waliopitia muda huo walishangaa kumuona mtu mfano wa Samaki aina ya Nguva, kumbe alikuwa ni mkurugenzi wao.

Mavi yam ganga Mengi yameendelea ya kushirikisha waganga wa ukweli na uwongo kupitia matapeli wa mumo humo bandarini.

Natamatia na kisa kingine cha aibu na kupotosha cha mmoja wa meneja mwingine pia wa KPA ambaye licha ya kuwa amestaafu leo, vile vile aliingia mtego huo wa ushirikina.

Kwa kuwa majuto ni mjukuu, hutokea baada ya kitendo kutendeka, anasema aliangukia mtego wa matapeli wa ushirikina humo ndani na jinsi alivyotaka kuzimiwa kesi yake ya kazi iliyomkabili.

Yeye anasema alipelekwa kwa mganga na baadhi ya wafanya kazi wa chini, mahiri mno kwa uganga. Yeye, aliambiwa wafuatane na mganga hadi kwenye mti wenye matawi panda mbili.

Kufi ka hapo baada ya kuhudumiwa kienyeji, anakumbuka aliambiwa asimame chini ya panda za mti ule ambazo ziligeuzwa kuwa shimo la choo cha uganga siku hiyo.

“Niliambiwa nisimame chini ya panda za mti huo huku mganga akipanda na kusema kwamba atahudumu chou kikubwa nami nipokee kinyezi chake moja kwa moja mikononi mwangu na ninuse akinihakikishia kwamba, kikinuka, kesi haitaisha lakini kikiwa bila hata harufu, nijue kutoka hapo sitasikia tena kesi yangu”, akumbuka afi sa huyu ambaye hakutaka kutajwa.

Share this story
Governor Sonko suspends 'super' CEC Kerich over school tragedy
Nairobi governor Mike Sonko has suspended 16 county officials following Monday accident, which left eight pupils dead, and a number injured.
China rejected Kenya's request for Sh32.8b debt moratorium
China is Kenya’s largest bilateral lender with an outstanding debt of Sh692 billion.
.
RECOMMENDED NEWS
Feedback