SECTIONS

HELB yatoa msamaha wa asilimia mia moja kwa wanafunzi wenye madeni

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB) imetangaza msamaha wa asimilia mia moja kwa wanafunzi wanaodaiwa madeni ya HELB baada ya masomo yao kufadhiliwa.

Afisa Mkuu Mtendaji wa HELB, Charles Ringera ametoa tangazo hilo akisema msamaha huo wa asilimia mia moja ya adhabu umetolewa kufautia athari za janga la COVID-19 kwenye uchumi.

Aidha, Ringera amesema msamaha huo umetolewa kupitia mpango wa Kamilisha Malipo Ya HELB' ambao utaendelea hadi tarehe 30 Aprili mwaka huu.

Hatua hiyo inalenga kuwahamasisha waliokopewa mikopop kulipa madeni ili kuruhusu bodi hioyo kuwanufaisha wanafunzi wengine

Vilevile, amebainisha kwamba COVID-19 iliathiri uchumi na kusababisha ukosefu wa ajira, changamoto za kibiashara na uhaba wa fedha hivyo kuathiri mpango wa HELP kufadhili masomo ya wanafunzi.

Bodi ya HELB iliwahi kutoa msamaha wa asilimia 100 mwaka 2013 ambapo wanafunzi 10, 110 walionufaika walilipa shilingi bilioni 1. 3.

Mnamo mwaka wa 2018, shughuli hiyo ilileta mapato ya shilingi milioni 870 kutoka kwa wanafunzi 9,998 walionufaika.