Kieleweke, Tanga Tanga ni mbolea ya ufisadi

Mbunge wa Jubilee Maina Kamanda akiongea katika kanisa la Katoliki eno la Ol Jaoro Rok Catholic church na Mbunge wa Kapseret MP Oscar Sudi ambaye ni mfuasi sugu wa Naibu Rais William Ruto na timu ya Tanga Tanga.

Yalianza kama makundi yenye misimamo kinzani ya kisiasa nchini, lakini kadri muda ulivyosonga, siku zika pita, Kieleweke na Tanga Tanga yakaibukia kuwa makundi mawili ya kisiasa tajika yaliyo kita mizizi katika ulingo wa kisiasa huku kila upande ukijitahidi kunadi sera zake ili kuwashawishi wananchi kuwaunga mkono.

Mwaka uliopita baada Rais Uhuru Kenyatta na aliye kuwa waziri mkuu Raila Odinga kukubaliana kufanya kazi kwa pamoja maarufu kama ‘Handisheki’ mirengo miwili ya kisiasa ikabuniwa.

Mrengo wa “Kieleweke” moja unaounga mkono mapendekezo ya juhudi za kuwaunganisha wakenya - Building Bridges Initiative maarufu BBI na mwingine unaojulikana kama “Tangatanga” unaopinga mabadiliko ya katiba kubuni nafasi zaidi za uongozi na badala yake kumpigia debe Naibu wa Rais Dr. William Ruto kutwaa uongozi wa taifa mwaka wa 2022.

Wafuasi wa Tangatanga wanahoji kwamba Ruto anamwakilisha mwananchi wa kawaida aliyeibukia uongozi bila kuwepo misingi ya uongozi katika familia yake tofauti na wanasiasa wengine ambao wanaonekana kurithi uongozi ulioachwa na baba zao.

Tofauti na kundi la ‘Tangatanga’, mrengo wa Kieleweke unapinga harakati za Ruto za kujipigia debe kwa kuzuru sehemu mbali mbali za nchi kukagua miradi ya maendeleo na kutoa michango ya fedha kwa makanisa kila jumapili ya wiki.

Wakereketwa wa kundi la “Kieleweke” wanadai kuunga mkono muungano wa Kiongozi Wa Upinzani Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta na ajenda Nne za maendeleo za serikali ya Jubilee.

Aidha wana “Kieleweke” hawajajitokeza kumuunga mkono muwaniaji wa kiti cha urais mwaka 2022 kinyume na mrengo wa Tanga Tanga ambao tayari wametangaza hadharani kutolegeza mwendo katika harakati za kumpigia debe mgombea wao Dr. william Ruto maarufu ‘Hustler’.

Msisimko huo wa makundi yenye misimamo mikali kuhusu hatima ya uongozi wa nchi umeendelea hadi kufi kia kiwango cha wanachama kuziwasilisha majina ya makundi la “Tangatanga” na “Kieleweke” kusajiliwa kama vyama vya kisiasa.

Makundi haya mawili hata hivyo yalipata pigo baada ya msajili wa vyama vya kisiasa Anne Nderitu kukataa kuyasajili makundi kutokana na sababu kwamba majina yalioyo pendekezwa yanakiuka kifungu 91 cha katiba kinachoeleza jinsi majina ya vyama yavyotakiwa kuchaguliwa, badala yake msajili huyo  akawataka kuwasilisha majina mengine kufanyiwa ukaguzi.

Wana kieleweke kutoka eneo la bonde la ufa nyumbani kwa Naibu wa Rais Dr. William Ruto wakiongozwa na mbunge wa Cherangani Joshua Kutuny wamekuwa kero kwa wafuasi  sugu wa Jubilee wanaomuunga mkono Naibu wa Rais Dr. William Ruto, Mara nyingi wamelauiwa kwa kutuhumiwa na wapinzani wa Ruto  kumpiga vita nyumbani kama njia moja ya kuziyumbisha nguzo zake muhimu katika azma yake ya kutafuta uongozi wa nchi.

Wafuasi wa Timu “Tangatanga” kutoka eneo la mlima Kenya wanalaumiwa kwa  kuigawa jamii ya eneo hilo katika makundi mawili na kupunguza ushawishi na mpango wa Rais wa kuyaunganisha makabila yote.

Wabunge wafuasi wa Timu “Tangatanga” wamesutwa kutokana na hatua yao ya kuendelea kumpigia debe Ruto hata badala ya ya kiongozi wao amabye ni Rais Uhuru Kenyatta ambaye anatarajiwa kuwapa mwelekeo wa kisiasa mwaka 2022.

Kundi la “Tangatanga” limewakashifu wanachama wa Kieleweke kwa kukosa ajenda na badala yake kujishughulisha kuhakikisha kwamba Ruto hafanikiwi kuingia Ikulu mwaka 2022 Chama tawala cha Jubilee kimeathirika sana kutokana na migawanyiko kati ya wabunge wafuasi wa makundi ya Tangatanga na Kieleweke huku wakati mwingine wakitatiza juhudi za serikali za kubambana na ufi sadi.

Wafuasi wa makundi hayo mawili wanatumia jukwaa la kisiasao kupinga au kuunga mkono jinsi taasisi za kupamabana na ufi sadi zinavyotekeleza majukumu yao ya kikatiba.

Ingawa demokrasia ya Kenya inaruhusu uhuru wa maoni na misimamo miongoni mwa washindani wa kisiasa, wanachama wa Kieleweke na Tangatanga hawajatumia fursa hiyo kuendeleza maendeleo bali ni kushughulikia hatima yao ya kisiasa baada ya Rais Uhuru kustaafu.

Siasa za kumrithi Rais Uhuru Kenyatta zimetekwa na makundi haya mawili huku ikiwa imepita miaka miwili pekee katika kipindi cha miaka mitano.

Wadadisi wa kisiasa wanasema ni mapema mno kwa siasa za uchaguzi mkuu wa mwaka 2022  ingawaje kama desturi tangu utawala wa vyama vingi vya kisasa, siasa za uchaguzi unaofuata  zimekuwa zikianza punde tu baada ya Rais kuapisha.