Seneta Moi atawazwa mzee Kalenjin

Seneta Gideon Moi avalishwa taji rasmi la kuwakilisha jamii ya Kikalenjini. [Picha: Standard]
Michemko ya siasa za kumrithi Rais Uhuru Kenyatta inazidi kushika kasi katika eneo la Bonde la Ufa nyumbani kwa Naibu wa Rais Dkt. William Ruto baada ya Seneta wa Baringo, aliyepia mwenyekiti wa chama cha KANU Gideon Moi, kuvikwa taji la kitamaduni na kutawazwa kuwa mzee wa jamii ya Wakalenjin. Kwenye ha? a iliyofanyika siku ya Jumamosi katika eneo la Mlima Elgon, Mwana wa Rais Mstaafu Daniel arap Moi, Gideon Moi alisimikwa kuwa mzee wa jamii ya Kalenjin.

Ni katika sherehe ambayo hufanyika baada ya mashauri na maelekezo kutoka kwa wazee wa Kikalenjin. Ha?a ya usimikaji hufanyika tu pale ambapo wazee wa jamii wanapopata ufunuo maalum na hupewa kiongozi aliye na nyota na ari ya kuongoza jamii kwa ujumla na wala sio jamii yake ndogo ama ukoo anakotokea kuamua. Eneo la Mlima Elgon linaaminika kuwa ndilo chimbuko la Jamii ya Wakalenjin kihistoria kwani inasadikika kwamba jamii hiyo iliingia Kenya kupitia mlima huo ulioko kaskazini Magharibi mwa nchi. Jamii ya wakalenjin pia inaamini kuwa sauti ya mababu zao imesalia katika mlima huo na kila jambo linalohusu uongozi wa nchi lazima litokee katika mlima huo kabla ya kutangazwa ama kupokelewa kwingineko zinakopatikana kabila tisa za jamii ya Wakalenjin.

 Kiongozi anayeteuliwa anatwikwa Jukumu la kutoa mwelekeo wa kisiasa kwa wanajamii, anaruhusiwa pia kufanya mazungumzo ya kubuni muungano na mara? ki wake wa kisiasa kwa niaba ya jamii ili mradi tu muungano ujali masilahi yake kwa kuangazia maswala ya Ukulima na ufugaji kwa kina,mambo hayo mawili ndio uti wa mgongo wa wananchi wa eneo la Bonde la Ufa. Wadadisi wanahoji kwamba kila mwanasiasa aliyetawazwa kwenye ha? a hiyo ya kitamaduni ameinukia kutwaa uongozi wa nchi. Mwaka wa 1962 sherehe za kumtawaza Rais msataafu Daniel Moi kuwa mzee wa jamii ya Wakalenjin zilifanyika eneo la Kapkatet Kaunti ya Nandi na hatimaye Moi akawa Rais wa Pili wa Jamhuri ya kenya baada ya Mwanzilishi wa Taifa Hayati Mzee Jomo Kenyatta kuaga dunia mwaka 1978.

Tangazo Maalum la mwaka 2007 linalofahamika kama “Elda Maravin Declaration” lililotolewa na Mbunge wa zamani Musa Sirma na kumtangaza Ruto kuwa anatosha kuwania kiti cha urais lilimuinua Naibu wa Rais William kisiasa na kupelekea kutawazwa kuwa mzee wa Jamii ya Wakalenjin katika Mji wa Eldoret na kuwa mwakilishi wa chama cha ODM katika eneo zima la Bonde la Ufa kabla na baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Ruto aliweza kufanikisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika chaguzi za miaka ya 2013 na 2017 mtawalia. Miaka 12 baadaye Bwana Sirma amerejea na Tamko linaloonekana kuchochea safari ya kisiasa ya Seneta Gideon Moi na ku? kia azimio lake la kuliongoza Taifa.

 “Kama jamii tuko tayari kuchukua mkondo mpya wa kisiasa katika eneo la Bunde la Ufa,” alisema Bwana Sirma, ambaye anaonekana kulihama kundi linalompigia upatu Naibu wa Rais William. Kutawazwa kwa Gideo Moi kuwa Kiongozi wa Jamii ya Wakalenji kumeanza kuzua tumbojoto kwa wafuasi wa Naibu Rais Dr. William Ruto na ni bayana kwamba hatua hiyoitaigawanja Jamii ya Wakalenjin mafungu mawili. Tangu mwaka 2018 Bwana Musa Sirma anayejulikana sana kama muandalizi wa Mfalme wa Jamii ya Wakalenjin ameonekana kutofautiana kisiasa na Naibu wa Rais Dr. William Ruto.

Bwana Sirma amelalamika mara kuwa Naibu wa Rais haaminiki tena kisiasa na ametangaza hadharani kuwa Seneta Gideon Moi ni chaguo lake la wadhifa wa Urais mwaka 2022. Hata hivyo bado inasubiriwa kama Seneta Moi atatoa tangazo la kutaka kumrithi Rais Uhuru Kenyatta ambaye ameonekana akifanya mazungumzo na vigogo wengine wa kisiasa na hata kuwaalika nyumbani kwake Kabarak. Kwa Wengi ni bayana kwamba Naibu wa Rais Dkt. William Ruto anatarajiwa kutwaa hatamu za uongozi kutoka kwa Rais Kenyatta.

Rais kenyatta anatarajiwa na wafuasi wa Ruto kuregesha mkono kwa kuwarai wapigakura kutoka jamii za Jamii ya Eneo la Mkoa wa Kati na Mashariki mwa nchi kumuunga mkono na kumpigia kura kwanjia kwa wingi. Tofauti na ilivyokuwa mwaka 2013 ambapo jamii ya Wakalenji ilishirikiana na jamii ya Wakikuyu kumchagua Uhuru Kenyatta kwa ushirikiano, wakati huu ni tofauti kwani hata Uhuru mwenyewe licha ya kuahidi kumuunga mkono Naibu wake baada ya kumailisha kipindi chake hajaonyesha dalili au kutoa tena tamko kama hilo wakati huu kipindi chake kinapoelekea kukamilia.

For More of This and Other Stories, Grab Your Copy of the Standard Newspaper.  

Aidha mkondo huu unaonekana vigumu kuziweka pamoja kura za jamii ya wakalenjin na jamii zinginezo kutoka eneo la Bonde la Ufa hasa baada ya Ujio wa Seneta Moi katika ulingo wa siasa za kitaifa na kupata uungwaji mkono kutoka kwa wabunge wa chama cha KANU na baadhi ya wale wa Jubilee, ODM na Wabunge wastaafu kwa mda mfupi.

 Kinyanganyiro cha kuwania kura za Bonde la ufa kinatarajiwa kuleta mchecheto zaidi baina ya makundi hayo mawili yanayo waunga mkono vigogo wa jamii ya Wakalenjin, Seneta Gideo Moi ambaye anaungwa mkono na wana wa mara? ki wa babake Rasi Mustaafu Moi na Naibu wa Rais Dr. William Ruto ambaye anaungwa mkono na wanasiasa waliojizatiti wenyewe ku? kia vilele vya kisiasa wanaojitambulisha kuwa “Hustlers” kama yeye. Kibarua ni kwa Naibu Rais William Ruto ambaye ngome yake inaonekana kupasuka katikati huku akijaribu kuibebeleza jamii ya Mkoa wa Kati kumuunga mkono kwenye kinyanganyiro cha mwaka 2022.

Do not miss out on the latest news. Join the Standard Digital Telegram channel HERE.

Get the latest summary of news in your email every morning. Subscribe below

* indicates required
Seneta Gedion MoiWilliam RutoUhuru Kenyatta