Gavana wa Machakos, Alfred Mutua ameikosoa serikali kutokana na hali duni ya makavazi ya kihistoria.

Gavana wa Machakos, Alfred Mutua ameikosoa serikali kutokana na hali duni ya makavazi ya kihistoria.

Akizungumza hapa jijini Nairobi baada ya kuzuru sanamu ya Tom Mboya na Dedan Kimathi, Mutua ameelezea kushangazwa kutokana na hali ya sanamu hizo, akisema serikali imetelekeza jukumu lake la kutunza na kurekebisha maeneo hayo.

Mutua aidha amesema atajukumika kukarabati na kuboresha hali ya sanamu hizo ili kuiweka historia miongoni mwa vizazi kuhusu viongozi wa awali wa taifa hili.

Amewakosoa wandani wa Rais Uhuru Kenyatta kwa kuendeleza siasa za mapema za mwaka 2022 badala ya kushirikiana na kulinda maeneo hayo ili kuboresha uongozi wa serikali.