Kimemia awaagiza maafisa wa usalama kuzifunga baa zote

Gavana wa Nyandarua Francis Kimemia amewaagiza maafisa wa usalama kuzifunga baa zote zinazohudumu kwneye kaunti hiyo bila leseni. Kimemia amesema baa hizo zimesababisha kuongezeka kwa idadai ya vijana wanaojihusisha na unywaji pombe vile vile matumizi ya dawa za kulevya.

Akizungumza katika Shule ya Upili ya Ol-Jororok Kimemia aidha amesema hali hiyo imechangia matokeo duni wakati wa mitihani ya Kitaifa.

Wakati uo huo, amewashauri viongozi wa eneo hilo kutafuta njia za kufadhili masomo hasa kwa wanafunzi werevu kutoka familia maskini akisema wengi wamelazimika kusitisha masomo yao kutokana na ukosefu wa karo.


Mbali na hayo ametoa wito kwa wazazi kujihusisha kikamilifu katika malezi ya wanao ili kuwasaidia kujiepusha na masuala yanayoweza kuyaathiri maisha yao kama vile mahusiano ya kimapenzi wakiwa wangali wachanga

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

Francis kimema