watatu wakamatwa mtaani Buruburu kulibomoa kanisa la CITAM

watatu wakamatwa mtaani Buruburu kulibomoa kanisa la CITAM. Watatu hao wamekamatwa wakati Gavana wa Nairobi Mike Sonko alipofika eneo hilo na kufanikiwa kuzuia ubomozi huo.

Waliokamawa wanadaiwa kukodiwa na bwenyenye mmoja anayedai kuwa kipande hicho cha ardhi ni chake. Polisi walifanikiwa kupata silaha kutoka kwa washukiwa hao zikiwamo panga .

Akizungumza katika eneo hilo, Sonko ameapa kwamba atahakikisha haki imetendeka na kwamba iwapo kuna watu wanaohusika na unyakuzi wa ardhi hiyo watachukuliwa hatua.

Gavana Sonko sasa ametoa wito kwa Inspekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai kuwachukulia hatua baadhi ya maafisa wa polisi waliokuwa wameandamana na washukiwa  ili kuwapa ulinzi.

Amedai mshukiwa wa unyakuzi wa ardhi hiyo anajulikana na anatumiamaagizo ya mahakama kuwadhulumu wamiliki halali.

Washukiwa hao Stephen Ouma, Alex Matheka na Peter Mulama wataendelea kuzuiliwa hadi Jumatatu watakapofikishwa mahakamani.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.