Polisi wanasa magunia kumi na mawili yaBangi Makueni.

Maafisa wa polisi wa eneo la Kibwezi kaunti ya Makueni wamenasa bangi magunia kumi na mawili katika sehemu ya Tsavo kwenye barabara ya Mombasa- Nairobi. Bangi hiyo ilikuwa ikisafirishwa kuelekea Mombasa kwa kutumia gari ya binafsi usiku wa kuamkia leo.

Naibu Kamanda wa Polisi wa Kibwezi Geoffrey Nderitu amesema maafisa wa trafiki wa Mtito Andei walishuku gari hilo kuwa na bangi kutokana na harufu, na waliposimmisha dereva akakaidi amri na akaongeza kasi, lakini alipokaribia eneo hilo la Tsavo, akazuiliwa na akaacha gari hilo kisha akatoroka.

Gari hilo limepelekwa hadi kituo cha polisi cha Mtito Andei huku dereva huyo akitafutwa. Nderitu ameonya kuwa watu wanaosafirisha bangi wanatumia magari ya kukodi, na watanaswa hukimbia na kuyaacha. 

Register to advertise your products & services on our classifieds website Digger.co.ke and enjoy one month subscription free of charge and 3 free ads on the Standard newspaper.

rolls of bhang