Polisi Auliwa kwenye Mtaa wa Umoja, jijini Nairobi

Polisi wanaendeleza uchunguzi baada ya mwenzao kupatikana akiwa amefariki dunia nyumbani kwake katika  Mtaa wa Umoja, jijini Nairobi. Afisa huyo kwa jina Hellen Kwamboka anayehudumu katika Kituo cha Polisi cha Bunge, alianza kutafutwa baada ya kukosa kuripoti kazini huku simu zake zikiwa zimezimwa.

Polisi walilazimika kuuvunja mlango wa nyumba yake baada ya kubaini ulikuwa umefungwa. Mwili ulipatikana ukiwa na majeraha kichwani huku kukiwa na dadili kwamba alikuwa amenyongwa.

Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa huenda aliuliwa na mpenziwe kwani ndiye mtu wa mwisho aliyemtembelea nyumbani kwake. Simu yake bado haijapatikana.

Kisa hiki kimejiri siku chache tu baada ya afisa mwingine wa polisi kwa jina Pauline Wangari kuuliwa katika Kaunti ya Murang'a. Polisi wanamzuilia mwanamume kwa jina Joseph Ochieng anayehusishwa na mauaji yake.

Register to advertise your products & services on our classifieds website Digger.co.ke and enjoy one month subscription free of charge and 3 free ads on the Standard newspaper.

Police Murder