EACC waendelezauchunguzi kwenye kaunti ya Kilifi.

Maafisa wa Tume ya Maadili na Kukabili ufisadi, EACC wanaendelea kuwachunguza maafisa sita wa serikali ya Kaunti ya Kilifi waliokamatwa jana kwa kuhusishwa na ufisadi.

 Maafisa hao wanakabiliwa na tuhuma za kukiuka sheria za ununuzi wakati wakati walipoidhinisha kununuliwa kwa boti la kuendeleza oparesheni za uokoaji baharini kwa kima cha shilingi milioni 14.8.

Miongoni mwa maafisa hao ni Afisa Mkuu wa Masuala ya Biashara na Utalii, Patience Tsimba, Mkurugenzi wa  Uvuvi, John Mwangi, mhasibu, Sophie Mmyamai Mwandawiro, afisa wa ununuzi, Mwaidza Munga, na afisa wa zamani wa kaunti hiyo Mohammed Silas Chuba. Mwingine aliyekamatwa ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Capital Solutions, Serah Musyimi.

Register to advertise your products & services on our classifieds website Digger.co.ke and enjoy one month subscription free of charge and 3 free ads on the Standard newspaper.