Shughuli ya usajili katika Mpango wa Huduma Namba inakamilika leo

Shughuli ya usajili katika Mpango wa Huduma Namba inakamilika leo hii kote nchini. Ikumbukwe wiki iliyopita Rais Uhuru Kenyatta aliongeza muda huo hadi leo baada ya kubaini kulikuwa na idadi kubwa ya watu ambao bado walikuwa hawajasajiliwa.

Shughuli hiyo imeratibiwa kukamilika saa kumi na mbili jioni. Hata hivyo usajili utaendelea katika ofisi za machifu japo kwa kuambatana na ratiba zao.

Msemaji wa Serikali Kanali Cyrus Oguna alisema, baada ya usajili kukamilika rasmi shughuli nyingine ya kutathmini data itafanyika, ili kuhakikisha kuwa taarifa kuwahusu wote waliosajiliwa zinaendana na stakabadhi zao.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

huduma namba registration