Serikali yazindua kitengo maalumu cha kukabili majanga katika KDF.

Serikali imezindua kitengo maalumu cha kukabili majanga katika Jeshi la Ulinzi, KDF yaani Disaster Management Unit ili kuhakikisha majanga yanakabiliwa kikamilifu nchini.

Akiwahutubia wanahabari jijini Nairobi, Waziri wa Ulinzi, Rachael Omamo amesema kitengo hicho kitasaidia katika kutoa ulinzi nchini na nje ya nchi.

Wakati uo huo, Waziri Omamo amewapongeza washikadau katika sekta mbalimbali kwa kuonesha ushirikiano wa hali ya juu taifa linapokabiliwa na majanga nchini.

<AUDIO>9669

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Sicily Kariuki ameipongeza idara ya KDF kwa kushirikiana na sekta ya afya wakati wa majanga. Waziri Kariuki amesema masuala ya afya na usalama yanapaswa kuzingatiwa hasa ikizingatiwa ukosefu wa usalama na afya bora kwa wote huchangia pakubwa kudorora kwa uchumi nchini.

Omamo aidha ametoa wito kwa Wakenya kuchukulia suala la ukosefu wa usalama kwa uzito linalokabili kila taifa wala si Kenya pekee. Vilevile amewashauri viongozi wa mataifa ya Bara la Afrika na Ulaya kulifanya kipaumbele suala la usalama ili kuhakikisha ustawi wa maeneo.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

serikalikdfRachael Omamo