DCI yatumia kamera za CCTV kumnasa mshukiwa Nairobi

Maafisa wa Idara ya Upelelezi, DCI wamefanikiwa kumkamata mshukiwa wa tano ambaye ni miongoni mwa walionaswa katika kamera za CCTV wakimpiga mwanamume mmoja.

Mwanamume huyo kwa jina James Luambe Odete amekamatwa kwenye eneo la Kilimani, jijini Nairobi akiwa katika nyumba moja ambako amekuwa akijificha. Mshukiwa mwingine kwa jina Innocent Samba angali anasakwa na polisi.

Washukiwa wengine walifikishwa mahakamani siku ya Jumatatu wiki hii ambapo walikana mashtaka dhidi yao na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tatu kila mmoja.

Do not miss out on the latest news. Join the Standard Digital Telegram channel HERE.

Get the latest summary of news in your email every morning. Subscribe below

* indicates required