Edward Alukuma wa Shinyalu anakula zaidi ya mifuko sita ya unga kila siku

Edward Alukuma akiwa katika pilka pilka za kuonyesha kipaji chake cha kula. [Photo: Courtesy]
Huku watu wakibarikiwa na vipaji mbali mbali kama vile vya kuimba, kucheza, kuigiza na vinginevyo maarufu, Edward Alukuma mwenye umri wa miaka 38 ameajaliwa kuwa na kipaji cha kumeza ugali kisawasawa utadhania unausunda kwenye kibuyu ilhali ni tumbo lake.

Anakula zaidi ya kilo kumi na mbili (12) za ugali kila siku, sawa na kuramba mifuko sita ya unga wa ugali ama nusu bandali la unga yeye peke yake. Wengi wanashangaa iwapo wake ni utumbo wa kawaida wa mwanadamu ama ni mabomba sawa nay ale yapitishayo maji. Alukuma ambaye ni mwenyeji wa Buyokha kaunti ndogo ya

Shinyalu katika kaunti ya Kakamega, ni jamaa ambaye anacho kipaji cha pekee na anaweza tu kufananishwa na hadithi za vitabu vinavyofanyiwa somo la fasihi shuleni wakatu huu, za Tumbo Liliso Shiba. Huku majirani wake wakimkwepa wakati na majira ya chakula cha mchana kila anapopitia karibu na majumba yao wakidhani anaweza kukubali mwaaliko wa chakula chao, Edward kamwe hana roho ya ulafi kwani kilo za ugali anazomenya, humchukua muda kwa siku kuhisi njaa isipokuwa kuchapa makopo ya maji muda hadi muda.

Familia ya Alukuma Edward ambaye ni baba wa watoto watano na wake wawili anapata riziki yake kupitia kwa ufundi wa kurekebisha ama kutengeneza piki piki (boda boda) katika soko la Shinyalu. Licha ya kumaliza ama kuwa na uwezo wa kula ugali kutoka kwa mifuko sita ya unga wa sima, yeye hutumia dakika kumi tu kurarua kilo sita (mifuko mitatu ama kilo 6) akitumia kitoweo chake maarufu cha mayayi. Akizungumza na Pambazuko huku akibubujikwa na jasho jembamba baada ya kugega ugali wake huo bila ya kusaidiwa na mtu hata tonge moja, anasema kuwa licha ya kuwa anao uwezo huo ama kipaji hicho cha maajabu ya shibe, kwake anachukulia tu kama kipaji chake cha kawaida na wala haoni kuwa ni ajabu kwake.

Ingawa hivyo anaongeza kusema kuwa watu wasione kuwa anakula hivyo kila siku bali hufanya hivyo kama maonyesho yake ya talanta ya kuweza kufanya hivyo. “Kwangu hii ni talanta lakini watu wasinifikirie kuwa naweza kufanya hivyo kila siku kwani mimi ni mzazi nikiwa na watoto wa kusomesha na wake wangu wawili,” anazungumzia hali ya gharama ya maisha kwamba inambidi avumilie kiasi hata kama tumbo lake litanguruma kudai sembe kwa mazoea yake ya kujazwa ugali daima.

“Kibarua change cha kurekebisha piki piki na gharama ya maisha, imenilazimu kupunguza tabia ama zoezi la kubwagiza sembe kilo 12 kwa siku kwa sababu ya majukumu kama mzazi na bwana,” asimulia Edward Alukuma ijapo anasema wafadhili wanapojitokeza kutaka kuthibitisha talanta yake ya kula ugali mwingi huo, huwa hana budi kuonyesha talanta kwa gharama ya mashabiki wenyewe.

Kipaji cha kumeza Anajitetea  kwa kusema kuwa talanta hiyo aliigundua akiwa mwanafunzi wa darasa la nane katika shule ya msingi ya Mukulusu alikosomea na baadae alianza kujiunga na mashindano mbali mbali yaliyo kuwa yakifanyika kila mwaka katika shule za Muranda na Shinyalu. 

Kipaji chake wakati mwingine kinamlipa kwani huwa ni vigumu mtu kuamini anachoambiwa bila kutaka kuhakikisha na kwa hilo mashabiki wake hutega hela (Betting) ili Edward ashiriki zoezi hilo pesa ambazo huondoka nazo baada ya kumaliza kipimo alicho wekewa na mteja wake, na hata hivyo anauwezo wa kushiriki zoezi hilo zaidi ya mara moja kwa siku na hiyo ni maana kwamba anauwezo wa kula zaidi ya kilo (12kg) kwa siku.

Kipaji cha kula Katika soko la Shinyalu na maeneo karibu yake mara kwa mara mashabiki wanaomfahamu vyema na wale ambao wanahamu ya kumuona ana kwa ana akithibitisha talanta yake ya kula ugali kiasi cha mifuko mitatu ya unga wa sima ama kilo sita kwa dakika ya chini ya dakika kumi (10), hukusanya pesa za wale wanaoamini wanaweza na wala ambao wanaye shauku kwamba anaweza kwa muda anaowekewa.

Edward bila ya wasi wasi wowote, huwakejeli mashabiki kwa kuwaagiza kubwaga pesa fulani ndio aweze kuwaonyesha talanta hiyo na isitoshe wenye kumshawishi kufanya zoezi hilo la kula, ndio wanaosimamia gharama ya kununua unga (mifuko ya unga wa sima na mayai na upishi wa kusonga sima na mboga yake).

La kushangaza ni kwamba Edward wakati mwingine hulazimika kula ugali kiasi cha kilo 12 kwa siku (mifuko sita) kwa maonyesho yake hayo. Hapa anasema ijapo ni zoezi la pesa ama ambalo hawezi kurudi nyumbani bila kitu, anataja kama kuwepo na changamoto la kupumua na matembezi akisema kwani hata lori la mizigo pia huwa na kiwango chake cha shehena na inapozidi basi breki zake ni za kucunga mno.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

Edward AlukumaUgaliKilo 12Shinyalu