Mwili wa Ivy Wangeci aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Moi kusafirishwa hadi Thika nyumbani kwao kwa maandalizi ya Mazishi

Mwili wa Ivy Wangeci aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Moi mjini Eldoret unatarajiwa kusafirishwa hadi mjini Thika. Jamaa za marehemu wanasema mwili huo utaondolewa katika hifadhi ya hospitali hiyo, ambapo utasafirishwa hadi nyumbani kwao kwa maandalizi ya hafla ya mazishi.

Ivy aliuliwa na Naftali Kinuthia siku ya Jumanne kwa kukatwa na shoka. Mshukiwa ambaye aliyeruhiwa na watu waliokuwa na ghadhabu aidha anatarajiwa kufikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka ya mauaji, kwani hali yake ya afya imeimarika.

Kinuthia aliwaambia maafisa wa DCI wanaochunguza kisa hicho kwamba alikuwa akimpenda Ivy na kwmaba alikuwa ametumia fedha nyingi kwake ila hakumpenda alivyotaka.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

ivy wangeciChuo cha MoiMjini Eldoret