Jeshi la Sudan kutoa tangazo muhimu muda wowote kutoka sasa

Muda wowote kuanzia sasa Jeshi la taifa la Sudan linatarajiwa kutoa tangazo muhimu baada ya ripoti kuwa jeshi hilo limezingira makao makuu ya Rais Omar Al Bashir.

Kwa siku sita maelfu ya waandamanaji wamekita kambi nje ya makao makuu ya jeshi nchini humo.

Baadhi ya waandamanaji wamefika katika makao hayo wakiji tayarisha kwa sherehe, huku wengi wakiamini kuwa miaka ya kukandamizwa imeisha.

Vilevile inaaminika kuwa baadhi ya maafisa wakuu wa serikali wamekamatwa huku Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Kahrtoum umefungwa.

SEE ALSO :1 in 5 office mugs contain faecal matter

Maandamano hayo yakumtaka Bashir ajiuzulu yalianza kufuatia kupandishwa bei kwa bidhaa muhimu. Bashir amekuwa Rais wa taifa hilo kwa miaka 30.

Bashir akijiuzulu atakuwa Rais wa pili wa taifala Kaskazini la afrika kuondolewa mamalakani kufuatia maandamano mwaka huu. Wakwanza akiwa Abdelaziz Bouteflika wa Algeria

Register to advertise your products & services on our classifieds website Digger.co.ke and enjoy one month subscription free of charge and 3 free ads on the Standard newspaper.