Raila Odinga meeleza umuhimu wa usajili kwa mfumo wa kidijidali NIIMS.

Kinara wa Chma cha ODM  Odinga ameeleza umuhimu wa usajili kwa mfumo wa kidijidali NIIM kwa misingi kuwa hatua yenyewe itaiwezesha serikali kutumia rekodi ya taarifa hizo katika kukadiria bajeti yake.

Akizungumza mjini Likoni, Kaunti ya Mombasa, Raila amekariri umuhimu wa usajili huo ili kuiwezesha serikali kudumisha usalama kwa kukabili ugaidi na kuboresha huduma zake.

Aidha Raila amepuuza pingamizi za taasisi mbalimbali kuhusu usajili huo ikiwamo tume za kutetea haki za kibinadamu KNHRC na KHRC na Muungano wa Wanubi ambazo ziliwasilisha kesi mahakamani ya kupinga shughuli hiyo.

Raila ametumia fursa hiyo kuwakashifu wabunge hasa wandani wa Naibu wa Rais Dkt. William Ruto, wanaopania kuwasilisha mswada bungeni wa kupunguza majukumu ya Idara ya Upelelezi DCI na ile ya Mkuu wa Mashtaka ya Umma DPP, kufuatia mjadala wa iwapo tume ya EACC ndiyo inayofaa kushughulikia kesi za ufisadi pekee au la.

SEE ALSO :Raila’s renewed interest in South Rift votes and leadership

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

RAILAUFISADINIMMS