Rais Uhuru Kenyatta amefanya ziara isiyo ya kawaida hadi katika ofisi ya naibu wake, William Ruto

Rais Uhuru Kenyatta amefanya ziara isiyo ya kawaida hadi katika ofisi ya naibu wake, William Ruto iliyo kwenye Barabara ya Harambee, Jijini Nairobi. Wawili hao wameshiriki mazungumzo japo ajenda ya mazungumzo hayo haijabainika. Kikao hiki kimejiri wakati ambapo vuta ni kuvute imekuwa ikishuhudiwa baina ya wabunge wanaomunga mkono Ruto na wale wanaompinga.

Leo hii baadhi ya wabunge wa Jubilee wamedai kwamba baada ya Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Seneti, James Orengo kusema kwamba atawasilisha mswada wa kumbandua  Ruto, huenda anatumiwa na Kinara wa ODM, Raila Odinga.

Wakiongozwa na Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro, wabunge hao wamesema hatua ya Raila kushirikiana na Rais Kenyatta ilikuwa njama ya kukisambaratisha chama hicho.

Nyoro amesema tayari wamepata habari kwamba nia ya ODM ni kuhakikisha Ruto ameondolewa kwenye wadhifa wake ili Raila achukue wadhifa huo.

SEE ALSO :Kamanda hails Uhuru, Raila truce and supports BBI team

Ikumbukwe Orengo amekuwa akiwaongoza viongozi wa upinzani katika harakati za kutoa mashinikizo ya kung'atuliwa mamlakani kwa Naibu wa Rais, William Ruto. Orengo anadai kwamba Ruto amehusishwa pakubwa na sakata za ufisadi na kwamba haungi mkono vita dhidi ya ufisadi.

Do not miss out on the latest news. Join the Standard Digital Telegram channel HERE.

president uhuru kenyattadeputy president william ruto