Wabunge wa Jubilee wamesema Orengo anatumiwa na Raila kuwasilisha mswada wa kumng'atua Ruto mamlakani

Siku chache tu baada ya Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Seneti, James Orengo kusema kwamba atawasilisha mswada wa kumbandua Naibu wa Rais William Ruto mamlakani, sasa baadhi ya wabunge wa Chama cha Jubilee wamedai kwamba Orengo anatumiwa na Kinara wa ODM, Raila Odinga.

Wakiongozwa na Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro, wabunge hao wamesema hatua ya Raila kushirikiana na Rais Kenyatta ilikuwa njama ya kukisambaratisha chama hicho.

Nyoro amesema tayari wamepata habari kwamba nia ya ODM ni kuhakikisha Ruto ameondolewa kwenye wadhifa wake ili Raila achukue wadhifa huo.

Ikumbukwe Orengo amekuwa akiwaongoza viongozi wa upinzani katika harakati za kutoa mashinikizo ya kung'atuliwa mamlakani kwa Naibu wa Rais, William Ruto. Orengo anadai kwamba Ruto amehusishwa pakubwa na sakata za ufisadi na kwamba haungi mkono vita dhidi ya ufisadi.

SEE ALSO :Uhuru, ex-Italian PM Renzi night meeting sealed Itare dam deal

For the latest news in entertainment check out Sde.co.ke and Pulser.co.ke , for everything sports visit Gameyetu.co.ke and ladies we have you covered on Evewoman