Polisi huko Eldoret kwa ushirikiano na mashirika mengine wameharibu zaidi ya paketi 12,000 za pombe haramu.

Polisi huko Eldoret kwa ushirikiano na mashirika mengine wameharibu zaidi ya paketi 12,000 za pombe haramu aina ya simba waragi miongoni mwa aina zingine za pombe hiyo zilizonaswa katika nyumba moja katika mtaa wa Kapsoya viungani mwa mji wa Eldoret.
 
Naibu Kamishena katika Kaunti Ndogo ya Ainabkoi, Nobert Komora amesema kwamba pombe hiyo kutoka nchi jirani ya uganda yenye dhamani ya zaidi ya shilingi laki tatu ilinaswa kwenye msako ulioendeshwa katika mtaa huo na maafisa wa usalama.
 
Komora amesema kwamba wamemnasa mwanamke mmoja  anayeendelea kusaidia maafisa wa polisi kuwasaka wafanyi biashara wengine ambao inaaminika ndio wamiliki rasmi wa pombe hiyo.
Ikumbukwe kuwa mapema mwezi huu, maafisa wa polisi katika eneo la Naiberi viungani mwa mji wa Eldoret pia walinasa pombe haramu na sharubati isiyoafiki viwango vya ubora kwa matumizi ya binadamu.

Register to advertise your products & services on our classifieds website Digger.co.ke and enjoy one month subscription free of charge and 3 free ads on the Standard newspaper.

EldoretAlcohol