Lusaka:Ushirikiano baina ya Kenya na Rwanda unatarajiwa kuimarika zaidi kufuatia ziara ya Rwanda.

Spika wa Bunge la Seneti, Kenneth Lusaka amekamilisha ziara yake ya siku nne nchini Rwanda ambayo ameitaja kuwa ya kufana, kukiwamo kutiwa saini kwa mkataba wa maelewano kati ya mabunge ya mataifa haya mawili ambao ushirikiano na uhusiano wake unatarajiwa kuimarika hata zaidi.

Lusaka na mwenyeji wake ambaye pia ni Spika wa Bunge la Seneti la Rwanda, Bernard Makuza wamekubailiana kuwa wataendeleza uhusiano huo mzuri na kwamba watalenga kujadili masuala ambayo yatakuwa ya manufaa kati ya Kenya na Rwanda.

Kwa mujibu wa maafikiano hayo, mabunge yote mawili sasa yatabuni mikakati ya kuandaa warsha na makongamano ambayo yatawahisisha wafanyakazi wake pamoja na kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria na kiuchumi.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.