Wanaotumia barabara ya Naivasha Mai Mahiu washahuriwa kufuatia mtetemeko wa ardhi

Polisi wa trafiki wanawashauri watumizi wa barabara ya Naivasha Mai Mahiu kutumia njia mbadala baada ya sehemu ya barabara hiyo eneo la Mirera kupasuka kutokana na athari za mtetemeko wa ardhi jana usiku.

Aidha, Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu, KeNHA imewashauri maafisa wa trafiki kuhakikisha kuwa barabara hiyo inafungwa hususan eneo la Fay Amario huku wahandisi wake wakiendelea kutathmini hali ya barabara hiyo.

Watumizi wa magari ya binafsi wametakiwa kutumia barabara ya Kamandura - Limuru - Kinungi kuelekea na kutoka Naivasha huku magari makubwa kama vile matrela yakitakiwa kuendelea kutumia barabara hiyo japo kwa kuelekezwa na maafisa wa polisi

For the latest news in entertainment check out Sde.co.ke and Pulser.co.ke , for everything sports visit Gameyetu.co.ke and ladies we have you covered on Evewoman