Mombasa: Oparesheni Fagia Bunge Saini 104,682 zimekusanywa kufikia

Eneo bunge la Kisauni kwenye kaunti ya Mombasa linaendelea kuongoza kwenye shughuli ya ukusanyaji wa saini za kufanikisha lengo la kulivunja bunge la kaunti hiyo ambapo kufikia sasa jumla ya saini 21, 156 zimekusanywa.

Eneo bunge la Mvita linafuata kwani jumla ya saini 20, 718 zimekusanywa, eneo la Nyali saini 18, 521, Likoni saini 18, 176, Changamwe saini 15, 080 na eneo la Jomvu jumla ya saini 11, 031 zimekusanywa.
Takwimu ya vuguvugu kwa jina Oparesheni Fagia bunge linaloendeleza shughuli hiyo inaonesha kwamba jumla ya saini 104, 682 zimekusanywa kwenye maeneo bunge yote sita ya Kaunti hiyo.
Shughuli hiyo iliyozinduliwa siku kumi na tatu zilizopita na vuguvugu hilo inalenga kukusanya saini 200, 000 zitakazowasilishwa kwenye idara zinazohusika ili kulivunja bunge la Kaunti hiyo.

Muda wa wiki nne uliwekwa kutekelezwa kwa shughuli hiyo inayoongozwa na makarani mia moja na wasaidi watatu kwenye kila Wadi.

Vuguvugu hilo liloanzishwa na baadhi ya Wenyeji wa Mombasa waliotaja kuchukua hatua hiyo kwa madai kwamba baadhi ya wawakilishi wadi wamekuwa wakiingilia utendakazi wa maafisa wakuu wa Serikali ya Kaunti hiyo.

SEE ALSO :Pensioners turn to Kenya's DCI in new bid to recover Sh1.2b assets

Ikumbukwe tayari bunge la Kaunti hiyo liliipitisha hoja ya kumbandua ofisini Waziri wa Uchukuzi Tawfiq Balala kufuatia malalamishi yaliyoibuliwa na Mwakilishi wadi ya Jomvu kuu Athman Shebe ya Balala kuzembea kwenye majukumu yake huku mawaziri Edward Nyale wa Ardhi na Munyoki Kyalo wa Michezo wakisubiri kunolewa na msumeno huo.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.