Polisi mjini Kisumu wawasaka washukiwa watatu wa wizi

Maafisa wa polisi mjini kisumu wanawatafuta washukiwa watatu wa wizi walioivamia duka moja na kuiba shilingi milioni moja.  Washukiwa wanasemekana kuivamia duka la Kavirondo Fishnets Sundry and Hardware limited lililoko karubu na hoteli ya New Victoria Hotel mjini humo.

Inaarifiwa washukiwa waliokuwa wamejihami waliwatishia wafanyakazi pamoja na wateja kwa bunduki kabla ya kutekeleza wizi huo kisha kutoweka kwa pikipiki.

Register to advertise your products & services on our classifieds website Digger.co.ke and enjoy one month subscription free of charge and 3 free ads on the Standard newspaper.