Washukiwa sita waliokamatwa Jumanne wakiwa na shilingi bilioni mbili pesa bandia kufikishwa mahakamani leo hii.

Washukiwa sita waliokamatwa Jumanne wakiwa na shilingi bilioni mbili pesa bandia kufikishwa mahakamani leo hii.

Sita hao ambao ni Eric Adede, mmliki wa hifadhi ya binafsi Safe Box katika Benki ya Barclays tawi la Queensways, ambapo pesa hizo bandia zilikuwa zimehifadhiwa,  Ahmed Shah, ambaye anasemekana kuwa ni mwekezaji wa kigeni, Elizabeth Muthoni na Irene Wairimu watashtakiwa kwa tuhuma za ulaghai. Aidha wafanyakazi wawili wa benki hiyo waliokamatwa pamoja na washukiwa watafikishwa mahakamani wakiwa ndio mashahidi.

Hayo yanajiri huku makachero wa Idara ya Upelelezi DCI wakipata dhahabu ndani ya kijisanduku kimoja kilichokuwa ndani ya hifadhi hiyo ya binafsi  jana jioni. Katika msako ulioongozwa na Mkurugenzi wa DCI George Kinoti washukiwa wanne miongoni wa sita waliokamatwa Jumanne walifikishwa katika eneo hilo, kuhojiwa zaidi.

Maafisa wa kukabili ugaidi walihusishwa katika msako huo baaada ya DCI kushuku kuwa huenda kulikuwapo na vilipuzi ndani ya kijisanduku hicho ila ikapatikana kuwa ilikuwa dhahabu.

Tayari wafanyabisahara wawili wamerekodi taarifa katika makao makuu ya Flying Squad wakidai kulaghaiwa shilingi milioni 5.5 na washukiwa hao

Mkuu wa Kitengo hicho cha Flying Aquad Musa Yego aidha amewashuri Wakenya ambao wanashuku kuwa huenda wamelaghaiwa na washukiwa hao kujitokeza kurekodi taarifa.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

WashukiwaMahakamaniPesa bandia