Nimeishi na virusi vya HIV kwa miaka 26. Kuwa na HIV hakumaanishi mwisho wa maisha

Kwa muda mrefu virusi vya hivi vimehusishwa na ngono, kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja na kuchukuliwa kuwa ugonjwa wa aibu. Aidha mafunzo mbalimbali kuhusu HIV yametolewa ili kupunguza unyanyapaa na kuelimisha jamii kuhusu njia mbalimbali ambazo mtu anaweza kupata virusi hivyo, jinsi ya kujikinga na unavyoweza kuishi iwapo utaambukizwa. Nimezungumza na mwanamke wa miaka 26, Doreen Moraa aliyezaliwa na virusi vya HIV  Katika hali isiyo ya kawaida, babaye hakuwa na virusi hiivyo isipokuwa mamaye, kwa kiingereza discordant couple.

Wazazi wake waligundua kuwa Doreen ana virusi vya HIV alipokuwa na miaka minane baada ya kuugua tangu alipokuwa mchanga. Kwa vile wakati huo hazikuwapo dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo, ARV's alimeza dawa ya Septrin kwa muda.

 

Alipokuwa mdogo alitengwa sana na baadhi ya jamii, wengi wakimlazimisha kutumia vyombo tofuati vya kulia.

Doreen anaeleza kuwa aligundua ugonjwa huo si kama homa ya kawaida alipomaliza darasa la nane, akijiandaa kujiunga na shule ya pili. Kwanza alijiunga na shule ya kutwa akiwa eneo la Kericho kisha kulazimika kwenda shule ya bweni baada ya ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007-2008.

SEE ALSO :Pensioners turn to Kenya's DCI in new bid to recover Sh1.2b assets

"Shuleni kila mwanafunzi ambaye alikuwa na dawa, alishauriwa kuziwacha katika kliniki ya shule, lakini mimi singeweza kwani nilikuwa naogopa unyanyapaa. Hivyo shule zikifunguliwa wazazi wangu walikuwa wanzificha dawa hizo, kisha watanipa nikienda bweni baada ya msako.Wanafunzi walioniona nikimeza dawa nilikuwa nikiwaambia nia matatizo ya moyo ndio maana nameza dawa"

Doreen anaeleza kuwa hali yake ya HIV ilimfisha moyo alipokosa kufanya kozi alizotaka.

"Nilitaka sana kuwa mtangazaji wa redi, aidha nilipotafuta ushauri nilielezwa kuwa , utangazaji utaniweka katika hali mabyo mashabiki atataka kujua maisha yangu, na sikuwa tayari kuzungumzia hali yangu ya HIV. Kisha nikataka kuwa mhudumu wa denge yaani 'airhostess' nilipoenda katika chuo cha mafunzo hayo, mmoja wa wahudumu wa shule hiyo aliniambia kuwa sitafaulu katika taaluma hiyo kwani nilikuwa na alama usoni."

Baadaye wakati mtaalam wa miti-shamba kutoka Tanzania, maarufu Babu wa Loliondo alipopata umaarufu, Doreen alimshawishi mamaye na wakaelekea nchini humo kumwona. Matibabu hayo yalipofeli alisusia dawa kabisa.

SEE ALSO :At times, pay more attention to form than merely grammar

"Nilikuwa nikimeza tu dawa za kawaida kutuliza maumivu hadi nilipopata ugonjwa wa nimonia. Dktar aliponiuliza kwanini niliwacha kumeza dawa nilimweleza nilikuwa nimechoka, kumeza dawa kila siku kunachokesha hiyo ndio moja ya chngamoto tunazopitia."

Doreen aneleza kuwa aliamua kuzungumzia hali yake ya HIV, baada ya kumwandikia mhariri wa kituo kimoja cha habari. Mhariri huyo alimhoji kisha kuchapisha katika gazeti na katika mitandao ya kijamii, hatua ambayo iliweka wazi hali yake hata kwa rafikize amabo hawakujua alikuwa na virusi vya HIV.
 
"Rafiki zangu walinipigia simu,wengine wakishangaa kwanini sikuwaamini na kuwaeleza nilikuwa na virusi vya HIV."
 
Aidha, anasema hata baada ya baadhi ya watu mitandaoni kumkashifu na kusema anatafuta tu umaarufu, alijipa moyo kwani lengo lake ni kuhakikisha virusi vya HIV havipewi nguvu zisizostahili.
 
Hata hivyo ulifika wakati akamlaumu mamaye kwa kumpa virusi hivyo. " Tulikosana nyumbani, kisha kwa hasira nikamwambia mamangu, kama si yeye singekuwa na virusi hivi, nikakataka kadi ya kliniki na kuzitupa dawa zangu, nikiapa sitazimeza tena. Babangu ndiye alinishawishi kumeza dawa na kumsamehe mamangu.
Vilevile Doreen anaeleza dhana inayoaminiwa na wengi kuwa ukiwa na virusi vya HIV, basi unastahili kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu aliye na virusi hivyo.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, wanandoa au wapenzi walio na virusi vya HIV wanastahili kutumia kinga kwani kuna uwezekano wa kuambukizwa aina tofauti ya HIV yaani reinfection or superinfection.

Kuna aina mbili za HIV. HIV 1 na HIV 2, baadhi ya walio na aina zote mbili huwa wameambukizwa na aliye na aina tofauti na aliyokuwa nayo. Hivyo madaktari hushauri matumizi ya kinga ila tu wakati wawili hao wanataka kupata mtoto.

Na kabla kupata ujauzito, viwango vya virusi hivyo mwilini huangaliwa kisha daktari huruhusu tu washiriki ngono bila kinga, viwangu vya virusi yaani viral load vikiwa chini na wakati mwili wa mwanamke unajitayarisha kwa hedhi yaani ovulation.

Tangu kuanzishwa kwa matumizi ya ARV's, wengi walio na virusi vya HIV huishi maisha ya kawaida na hata kupata watoto wasio na virusi vya HIV.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.