Maraga kuwasilisha hoja ya kumbandua Jackton Onjwang kwa Rais Uhuru Kenyatta

Jaji Mkuu, David Maraga amethibitisha kuwa ataiwasilisha kwa Rais Uhuru Kenyatta hoja ya Tume ya Huduma za Mahakama, JSC ya kutaka Jaji wa Mahakama ya Juu Jackton Onjwang' aondolewe ofisini. Katika kikao na wanahabari muda mfupi uliopita, Jaji Maraga amesema JSC imewasilisha ripoti iliyo na maelezo ya kina kuhusu pendekezo lake dhidi ya Jaji Onjwang'.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya JSC, Jaji Onjwang' anatuhumiwa kwa ukiukaji wa sheria za Idara ya Mahakama na utumiaji mbaya wa ofisi. Aidha anatuhumiwa kwa kukaidi agizo la kumtaka afike mbele ya JSC kutoa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili. Sasa JSC inamtaka Rais Kenyatta kubuni jopo maalum kwa mujibu wa sheria kuanza mchakato wa kumwondoa ofisini jaji huyo.

For the latest news in entertainment check out Sde.co.ke and Pulser.co.ke , for everything sports visit Gameyetu.co.ke and ladies we have you covered on Evewoman