viongozi wa makanisa wamtaka Rais Kenyatta kuzidisha vita dhidi ya ufisadi.

Huku suala la ufisadi likizidi kuwa kero nchini, viongozi wa makanisa wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuzidisha vita dhidi ya janga hilo na wahusika wakabiliwe kisheria.
 
Muungano wa Kitaifa wa Makanisa ya Kipentekosti tawi la Mombasa, limesema changamoto zinazoshuhudiwa nchini zinasababishwa na watu wanaopora mali ya umma.
 
Askofu Nalo amezitaka idara za uchunguzi kuhakikisha wahusika wa uporaji wa mali ya umma wanakabiliwa kwa mujibu wa sheria.
 
Wakati huo, askofu huyo amepinga vikali hatua ya wabunge kutaka kubuni sheria za kudhibiti makanisa na baadhi ya wahubiri ambao wanawalaghai Wakenya pesa zao.
 
Kuhusu suala la wahubiri kuwa na shahada, askofu huyo amesema hakuna sheria inayomzuia yeyote kuhubiri au kuanzisha kanisa kwa kigezo cha elimu.
 
Haya yanajiri huku Mhubiri wa Kanisa la Neno Evangelism, James Ng'ang'a akikabiliwa na mashtaka ya kumtishia maisha mwanahabari wa Runinga ya Citizen, Linus Kaikai kufuatia kauli yake kuwa serikali inafaa kuwadhibiti wahubiri nchini ambao anasema asilimia kubwa wamekuwa wakiwalaghai wananchi mamilioni ya pesa.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

ufisadi