Washukiwa wa NYS kupokonywa mali

Kitengo cha Serikali cha Kurejesha Mali ya Umma sasa kinataka vipande vitano vya ardhi pamoja na magari matatu yanayomilikiwa na familia ya washukiwa wa sakata ya pili ya Taasisi ya Huduma kwa Vijana, NYS, Anne Ngirita kutwaliwa na serikali.

Katika ombi kwa mahakama litakalosikilizwa tarehe 15 mwezi Aprili mwaka huu, kitengo hicho kimesema kuwa ardhi na magari hayo yanaaminika kununuliwa kutoka kwa fedha za NYS zilizofujwa.

Ikumbukwe kuwa mali hiyo ilithibitiwa na serikali mwaka uliopita baada ya Jaji  Hediwg Ong’udi kushawishiwa kuwa ilinunuliwa na fedha hizo. Mali hiyo imehusishwa na Phyllis Njeri, Jeremiah Gichini Ngirita pamoja na mamayo Lucy Wambui Ngirita.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

NgiritaMali