Huenda shughuli ya kuwateua majaji ikasitishwa, baada wa wakili Adrian Kamotho kuwasilisha kesi kupinga shughuli hiyo

Kwa muda sasa kumeendelea michakato mbalimbali ya kushinikiza kura ya maamuzi, wa muhimu zaidi ukiwa ule unaoendelezwa na jopo la mapatano ambalo linakusanya maoni kuhusu njia bora zaidi ya kushughulikia changamoto za utangamano nchini

Huenda shughuli ya kuwateua majaji ikasitishwa, baada wa wakili Adrian Kamotho kuwasilisha kesi kupinga shughuli hiyo hadi wakili mwanamume kutoka Chama cha Mawakili LSK ateuliwe kwenye Tume ya Huduma za Mahakama, JSC. 

Kamotho anataka shughuli  ya kuwahoji majaji hao itakayofanywa na Mahakama ya Leba na Uajiri kusitishwa mara moja.

Uchaguzi wa wawakilishi wa kiume wa LSK umeratibiwa kufanyika tarehe 9 Mei. Kamotho amedokeza kwamba pasi na mwakilishi wa kiume kutoka LSK itakuwa vigumu kwa Tume ya Huduma za Mahakama kutimiza kipengele cha 14, ibara ya tatu na tano ya katiba. Wakili huyo amewataka majaji watakaoendesha shughuli hiyo kuzingatia sheria.

Jaji Mkuu David Maraga, alitangaza kwenye Gazeti Rasmi la serikali Januari 15, kwamba shughuli ya kutuma maomba kwa wanaotaka kuwania itafika mwisho leo juma tatu.

Wakili Tom Ojienda, ambaye ametuhumiwa kukwepa kulipa kodi ya shilingi milioni 400 ni miongoni mwa wengine watano ambao majina yao yamechapishwa kwa ajili ya kuhojiwa.

Do not miss out on the latest news. Join the Standard Digital Telegram channel HERE.