Waliofariki kufuatia ajali ya ndege Ethiopia, wafanyiwa mazishi

Maelfu ya Raia wa Ethiopia leo hii wamehudhuria hafla ya mazishi ya mapoja ya baadhi ya watu waliofariki dunia kufuatia ajali ya Ndege ya Ethiopian Airlines Jumapili iliyopita. Jamaa za watu kumi na saba walibeba jeneza kumi na saba  za waliofariki bila mili kwa maziko.

Hafla hii imeandaliwa siku moja tu baada ya jamaa hao kuruhusiwa kuubeba udongo kutoka eneo la mkasa kwa hafla hizo, baada ya kuarifiwa kuwa shughuli ya kuwatambua wapendwa wao huenda ikachukua muda. Familia za walioaga zinasema waliruhusiwa kubeba udongo kilo moja pekee.

Wakati uo huo, maafisa wa nchini Ufaransa wanaokichunguza kijisanduku maalum cha kurekodi data za safari za ndege yaani Blackbox, cha ndege iliyoanguka, walisema jana jioni wamefanikiwa kupata sauti zilizorekodiwa na kuziwasilisha kwa maafisa wenzao wa Ethiopia bila kuzisikiliza. Uchunguzi wenyewe umeendelea leo, japo taarifa zaidi hazijatoleewa.

Maafisa wa Idara ya Usafiri wa Angani wa Marekani na wale wa Kampuni ya Ndege ya Boeing ni miongoni mwa wanaohusika katika uchunguzi.

SEE ALSO :Ethiopian Airlines GCEO re-appointed to IATA Board of Governors

Ikumbukwe jana shirika la Ethiopian Airlines lilisema kuwa uchunguzi wa DNA utachukua kati ya miezi mitano na sita, japo jamaa za waliofariki dunia watapokezwa vyeti vya wafu kw akipindi cha wiki mbili zijazo.

 

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

EthiopiaWazikwaMazishi