Rais Kenyatta ametakiwa kujiuzulu endapo atashindwa kukabili ufisadi nchini

Rais Uhuru Kenyatta ametakiwa kujiuzulu wadhifa huo endapo atashindwa kukabili ufisadi nchini. Wito huo umetolewa na Wanaharakati wa Kutetea Haki za Binadamu chini ya mwavuli wa Goodwill, walioandamana leo  katika Bustani ya Uhuru, Jijini Nairobi.

Wanaharakati hao wameapa kuandamana nje ya ofisi ya Rais Kenyatta  kila wiki ,hadi mawaziri na maafisa wengine wa serikali wanaohusishwa na ufisadi watakapojiuzulu. 


Wanaharakati hao wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Elius Ngugi ,aidha wametoa wito wa ufisadi kutajwa kuwa janga la kitaifa huku wakiishtumu Idara ya Mahakama na Tume ya Maadili na Kukabili  Ufisadi, EACC kwa ongezeko la visa vya ufisadi nchini.

For the latest news in entertainment check out Sde.co.ke and Pulser.co.ke , for everything sports visit Gameyetu.co.ke and ladies we have you covered on Evewoman