Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, amemshtumu Waziri James Macharia kwa kuwataja kuwa wahalifu wafanyakazi wanaogoma JKIA.

Licha ya utulivu kurejea katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta kufuatia mgomo wa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, KAA hali ya switafamu inaendelea kutanda miongoni mwa abiria ambao safari zao za ndege zimetatizika kufuatia mgomo huo.

Wengi wangali katika uwanja huo wakisubiri kubaini hatma ya safari zao. Hayo yakijiri, Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, amemshtumu Waziri James Macharia kwa kuwataja kuwa wahalifu wafanyakazi wanaogoma JKIA. Amesema wanaogoma wana haki ya kutetea maslahi yao na yu tayari kuongoza maandamano hayo kuanzia kesho tarehe 7 Machi.

Owino aidha amesema hatalikubali pendekezo la serikali la kujumishwa kwa KAA na Shirika la Ndege la Kenya Airways, KQ akisema ilivyo sasa KQ imekuwa ikishuhudia hasara katika huduma zake. Mapema leo alipofika katika Uwanja wa JKIA, Waziri Macharia alisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wafanyakazi hao kwa kutatiza usalama katika eneo ambalo linastahili kuwa na ulinzi mkali.

For the latest news in entertainment check out Sde.co.ke and Pulser.co.ke , for everything sports visit Gameyetu.co.ke and ladies we have you covered on Evewoman