Abiria wote waliotarajiwa kusafiri kupitia JKIA lakini wangependa kuahirisha safari zao wameruhusiwa kufanya hivyo bila malipo

Abiria wote waliotarajiwa kusafiri leo lakini wangependa  kuahirisha safari zao wameruhusiwa kufanya hivyo bila malipo huku Shirika la Ndege la Kenya Airways kwa ushirikiano na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege yakijizatiti kurejesha hali ya kawaida katika uwanja wa JKIA.

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu Mtendaji wa KQ, Sebastien Mikosz, tayari baadhi ya abiria wameanza kukaguliwa kili kuondoka kwa safari za kuelekea Amstedam na London huku maafisa wa KDF wakitumwa kusimamia shughuli.

Hayo yanajiri huku Waziri wa Uchukuzi, James Macharia akisisitiza kuwa mgomo wa wafanyakazi wa viwanja vya ndege si halali japo umekabiliwa kwa wakati ili kurejesha shughuli za kawaida uwanjani.

Awali, katibu wa wafanyakazi hao alizungumza  kutoka kituo cha polisi cha JKIA kilalamikia kutiwa mbaroni bila sababu.

SEE ALSO :Uhuru, ex-Italian PM Renzi night meeting sealed Itare dam deal

Register to advertise your products & services on our classifieds website Digger.co.ke and enjoy one month subscription free of charge and 3 free ads on the Standard newspaper.