Maafisa wa polisi wawili wafariki dunia matuga

Mafisa wawili wa polisi waliokuwa wakihudumu kwenye Kituo cha Polisi cha Matuga kwenye Kaunti ya Kwale wamefariki dunia baada ya tuk-tuk waliyokuwa wakisafiria kugongwa na matatu ya abiria katika eneo la Waa saa chache zilizopita.

Kamanda wa Polisi eneo la Matuga Joel Chesire amesema kwamba wawili hao walikuwa wameabiri tuk-tuk hiyo kuelekea kazini.
 

Amesema kwamba wengine waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo akiwamo dereva wa Tuk-tuk wanatibiwa kwenye hospitaliti mbalimbali kwenye kaunti hiyo.

Mili ya wawili hao imelazwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya Coast General jijini Mombasa.

Do not miss out on the latest news. Join the Standard Digital Telegram channel HERE.