Watahiniwa wa KCPE na KCSE mwaka huu kuthibitisha usajiliwa wao kuanzia Jumatatu

Shughuli ya kutathimini watahiniwa waliojisajili kuifanya mitihani yao ya kitaifa ya Darasa la Nane KCPE na Kidato cha Nne KCSE itaanza rasmi kesho kesho. Baraza la Mitihani Nchini KNEC limesema shughuli hiyo itaendelea hadi tarehe 28 mwezi huu. Kulingana na KNEC hatua ya kuwapa watahiniwa nafasi ya kuthibitisha usajili wao  inalenga kurekebisha makosa ili kuhakikisha hakuna atakayekosa kuufanya mtihani huo.

Shughuli ya usaliji iliyoanza tarehe mbili mwezi huu ilikamilika tarehe kumi na tano yaani Ijumaa ambapo watahiniwa milioni 1.78 walikuwa wamesajiliwa kufanya KCPE na KCSE mwaka huu. Miongoni mwa waliosajiliwa watahiniwa milioni moja elfu thamanini na tisa mia sita sabini na moja watafanya KCPE huku elfu mia sita tisini na wanane mia tisa thelathini na watano wakisajiliwa kufanya KCSE.

Wazazi wameshauriwa kuthibitisha iwapo wanao wamesajiliwa kwa kutuma ujumbe mfupi  kwa nambari 20076. Afisa Mkuu Mtendaji wa KNEC Marcy Karogo amewashauri kuwasiliana na walimu wakuu iwapo kutakuwapona tatizo lolote. Amesisitiza kwamba muda wa kusajiliwa wa watahiniwa hautaongezwa.

Wakati uo huo, walimu wakuu wameshauriwa kuwapa nambari za usajili watahiwa kulingana na utaratibu kuhusu jinsi walivyojiunga na shule zinazohusika wala sio kulingana na matokeo yao ya mitihani jinsi ambavyo wamekuwa wakifanya. Aidha KNEC imewashauri watahiniwa kujisajili kwenye shule wanakosomea. 

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

WatahiniwaMitihani