''Serikali itaanza kuwalima wakulima wa miwa'' Amesema Ruto

Serikali inakamilisha mipango ya kuwalipa wakulima wa miwa wa eneo la Magharibi ya nchi. Naibu wa Rais William Ruto amesema shilingi bilioni 1.9 miongoni mwa shilingi bilioni 2.7 ambazo wakulima wanaidai serikali zitalipwa hivi karibuni katika awamu ya kwanza.

Ruto amesema pesa hizo zitalipwa moja kwa moja kwa wakulima na wala si kupitia viwanda.

Wakati uo huo amewasihi Wakenya kuungana bila kujali miegemeo yao ya kisiasa ili kufanikisha miradi ya maendeleo huku akisisitiza umuhimu wa viongozi kuungana katika kufanikisha maazimio ya serikali.

Akizungumuza alipohudhuria hafla ya mazishi ya Marehemu Peletina Washiali, Mamaye  Kiranja wa Wengi Katika Bunge la Kitaifa ambaye pia ni Mbunge wa Mumias Mashariki, Ruto ametumia fursa hiyo kuwarai viongozi kuiunga serikali mkono ili kufanikisha ajenda nne kuu ambazo ni Utoshelezo wa Chakula, Afya kwa Wote, Makazi Bora na Ukuaji wa Viwanda. Amesema serikali imetenga fedha katika sekta mbalimbali ili kupiga jeki miradi ya maendeleo.

Naibu huyo wa Rais amewakosoa viongozi wanaoendeleza siasa za mwaka wa 2022 akisema wanalirejesha taifa hili nyuma kimaendeleo.

Kwa upande wake Gavana wa Kakamega, Wycliffe Oparanya amewarai wakazi eneo la Magharibi ya nchi kuwaunga mkono viongozi wanaolenga kuwahudumia bila kujali misingi ya kikabili, dini na siasa.


 

For the latest news in entertainment check out Sde.co.ke and Pulser.co.ke , for everything sports visit Gameyetu.co.ke and ladies we have you covered on Evewoman

WakulimaMiwaKulipa