Mzozo wa kidiplomasia waibuka baina ya Kenya na Somalia

Mvutano wa kidiplomasia umeibuka baina ya Kenya na Somalia, baada ya Somalia kuyauza mabomba ya mafuta na gesi kwa njia ya mnada iliyo katika sehemu inayozozaniwa baina ya mataifa haya mawili. Kenya imemwagiza Balozi wa Kenya nchini Somalia generali mstaafu Lucas Tumbo kurejea nchini mara moja mwa mashauriano. Aidha Balozi wa Somalia nchini ameagizwa kurejea nchini mwao. Kamau Macharia ni Katibu wa Wizara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni.

Kamau amesema Somalia iliyauza mabomba hayo kwa mataifa ya Uingereza, Norway na Ireland Kaskazini tarehe saba mwezi huu, hivyo kukiuka mikataba ya kimataifa ya makuabliano kuhusu utatuzi wa mizozo ya mipaka na diplomasia.

Katibu huyo amesema serikali ya Kenya haitasalia kimya kulihusu suala hilo, akisisitiza kuwa Somalia imeonesha wazi kwamba haijakomaa kidiplomalia wala kisiasa. 

Mzozo wa umiliki wa sehemu hiyo inayozozaniwa umekuwapo kwa muda sasa. Ikumbukwe mwaka 2014, Somalia iliishtaki Kenya katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ. Kesi hiyo ilipingwa vikali na Kenya ambayo ilikuwa ikipendekeza njia mbadala ya kusuluhisha mzozo huo. Hata hivyo,  majaji wa mahakama hiyo, walikubali kesi hiyo ambayo ingali mahakamani kusikilizwa hadi iamuliwe.

SEE ALSO :Kenya shuts border with Somalia in Lamu

Eneo linalozozaniwa liko umbali wa kilo mita mia moja Mashariki mwa Pwani ya Kenya.

Kenya imekuwa mshirika mkuu wa Somalia hasa kuhusu juhudi za kuleta amani nchini humo vilevile kuwasaidia wakimbizi wanaotoroka taifa hilo kufuatia utovu wa uslama. Kuna zaidi ya wakimbizi elfu nne wa Somalia wanaoishi kwenye kambi nchini hasa ile ya Dadaab. Kambi hiyo imekuwa ikidaiwa kutumika na makundi ya kigaidi hasa Al-Shabaab kutekeleza mashambulio ncini.

Aidha Kikosi cha Ulinzi cha Kenya KDF kimekuwa nchini Somalia  tangu mwaka 2011, nchini ya AMISOM, kulikabili kundi hilo la Al-Shabaab. Kinachosubiriwa ni kuona hatua zitakazochukuliwa kufuatia hatua hiyo ya Kenya ikizingatia kwamba juhudi zake, kulitaka taifa la Somalia kuondoa ramani iliyotumia kuyauza mafuta na gesi hiyo inayoonesha kuwa eneo linalozozaniwa liko nchini humo hazijazaa matunda.

SEE ALSO :The unseen war - Part 2

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

SomaliaKenyaDiplomasia