Azma ya Joe Nyagah yaungwa mkono na wagombea huru wenzake

Na Rosa Agutu
"Tuna imani ya kuibuka washindi wakati wa uchaguzi mkuu kwa kuwa Wakenya wengi wamechoshwa na serikali ya sasa". Kauli hiyo imetolewa na aliyekuwa mshauri wa Rais Uhuru Kenyatta Joe Nyagah alipotangaza rasmi kuwania urais akiwa mgombea huru.
Nyagah amesisitiza kuwa Kenya inahitaji mabadiliko makubwa kwani hakuna tofauti kati ya Muungano wa NASA na Chama cha Jubilee. Vilevile ameshirikiana na wagombea huru wengine wanaounga mkono azma yake, ambao kwa pamoja wamesisitiza kwamba Kenya inahitaji uongozi mpya.
David Munga ambaye mmoja wa wagombea huru amesema wananchi wanafaa kumchagua kiongozi atakayeleta mabadiliko nchini, wala sio kwa kuzingatia chama au kabila.