Waititu aibuka mshindi katika uteuzi Kiambu

Na, Beatrice Maganga
‘’Niko tayari kuwatumikia wakazi wa Kiambu bila ubaguzi. Ndiyo kauli ya Mbunge wa Kabete Ferdinard Waititu punde alipotangazwa kuwa mshindi wa uteuzi wa ugavana kwa tiketi ya Chama cha Jubilee. Waititu amepata kura elfu mia tatu hamsini na tatu, mia sita na nne. Gavana wa sasa wa kaunti hiyo, William Kabogo amepata kura 69,916. Waititu amewapongeza wote waliompigia kura.
Aidha licha ya kumbwaga Kabogo katika uteuzi huo, Waititu amesema yu tayari kushauriana naye kuhusu masuala ya uongozi.
Wakati uo huo ameahidi kuhakikisha kuwa wananchi wanajumuisha katika masuala ya uongozi wa kaunti iwapo ataibuka msindi katika kinyang’anyiro cha Agosti nane huku akiwapongeza wakazi wa Kiambu kwa kuonesha ukomavu wa kisiasa na kuwachagua viongozi wanaowataka.
Wengine walioibuka washindi katika uteuzi wa Jubilee kwenye Kaunti ya Kiambu ni wabunge, Moses Kuria, Alice Ng'ang'a, Kimani Ichung'wa, Francis Waititu, Paul Koinange na Jude Njomo.