Sonko awaonywa wafanyakazi fisadi

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amewashtumu wale wanaoikosoa hatua yake ya kuwafuta wafanyakazi wa kaunti ambao ni fisadi. Sonko amesema ataendelea na uchunguzi na iwapo kuna wafanyakazi watakaohusishwa na visa vyovyote wa ufisadi wataachishwa kazi. Amesema jumla ya wafanyakazi sitini wametambulika na kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.

Wakati uo huo, amewaonya wawakilishi wadi anaodai wamelipwa ku mhangaisha ili aitimize lengo hilo.

Aidha ili kumaliza wizi wa dawa za hospitali za kaunti ya Nairobi, Sonko amesema kwamba serikali yake itaanza utaratibu wa kuziweka nembo maalum dawa zinazosambazwa katika hospitali hiyo ili kuzuia hali hiyo.

Gavana Sonko, pia ameitetea hatua ya kuyabomoa majengo inayoendelea jinini Niarobi. Kulingana na Sonko hatua hiyo inalenga kuimarisha hadhi ya mji huu. Hata hivyo amesema kwamba watu wote walioathirika na ubomozi huo watafidiwa. Aidha amewaagiza wawakilishi wadi wote themanini na tano kuwasilisha orodha ya waathiriwa ili kumwezesha kuwafidia.

Amesema majengo yaliyojengwa karibu na maeneo ya mito na mabomba ya kupitishia maji taka pia yatabomolewa.

 

Related Topics

Sonko Nairobi